SoC02 Hatukuandaliwa tukiandae kizazi chetu kubadilika

SoC02 Hatukuandaliwa tukiandae kizazi chetu kubadilika

Stories of Change - 2022 Competition

boyson onlye

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2015
Posts
1,108
Reaction score
1,397
Habari wakuu natumai ni wazima wafya

Poleni na majukumu ya kazi na mihangaiko ya hapa na pale

Niende moja kwa moja kwenye mada husika

Maisha yamekuwa hayatabiriki au hayaeleweki, yamekuwa na changamoto nyingi mpaka tunafika hatua ya kujuta kuzaliwa, unawaza sana pale unapopata changamoto na hatimae hupati muwafaka wa matatizo au changamoto zinazokukabili.

Mara nyingi tumefanya maamuzi mengi ya kijinga yanayopelekea kwenye majuto makubwa kwa sababu ya nyakati ngumu tulizopitia au tunazoendelea kupitia, kuna namna ambavyo tuliaminishwa kuhusu maisha hasa na wazazi au walezi wetu,

Wazazi au walezi wetu wengi wao wamekulia katika kipindi ambacho unatakiwa uwe na nguvu nyingi ndio uweze kumiliki mali hata ilipofika kipindi cha elimu hawakuhitaji elimu kubwa kufanya kazi katika wizara flani hivyo wakakua katika hayo mazingira mpaka pale nguvu ilipobadilika na kuhamia kwenye swala la elimu kwamba ukisoma basi unauhakika wa maisha, hapo ndipo wengi tumezaliwa na kukuzwa katika maneno hayo na mazingira hayo, ya ukifika chuo kikuu utakuwa na maisha mazuri, au ukisoma maisha yako yatabadilika

Uhalisia ni kwamba maisha yamebadilika sana Elimu inanafasi ila siyo kama ilivyokuwa inatarajiwa au inavyotarajiwa na wazazi wetu ya kuwa ukiwa na Elimu basi unauhakika wa maisha, maisha yanaelekea kwenye ujuzi zaidi maisha yanaenda mtandaoni zaidi, maisha yamemezwa na utandawazi na teknolojia, maisha yemkuwa yanauliza

Unaweza kuzalisha nini, unaweza kufanya nini, maisha yanatoka kule ambako zamani yalikuwepo ya kukuuliza unaelimu gani na yanaenda kwenye unaweza kufanya njni? Elimu ni ya muhimu lakini haitupi uhakika wa kuishi maisha tunayoyatarajia kuna wakati unatakiwa uweke vyeti ndani utumie akili yako uliyozaliwa nayo na kidogo ile uliyopata darasani,

Kwa nini utumie akili yako ya kuzaliwa zaidi?

Kwa sababu Darasani mmetoka wanafunzi zaidi ya 1000 na wote mmefundishwa kitu kimoja hivyo unatumia akili ya kuzaliwa zaidi ili kuweka utofauti wa kile unachofanya,ni wakati wa kuwafundisha watoto wetu tarajiwa kuwa wasome ila wasiache akili zao za asili kufanya kazi, tuwajulishe mapema kuwa maisha yanahitaji elimu zaidi ya ile tunayokaririshwa darasani, kila mmoja amesoma na ana elimu hivyo tuangalie ni nini kinamfanya yeye awe wa pekee, tuwahimize kusoma kwa bidii lakini pia tuwaangalie wanaweza kufanya nini baada ya Elimu,

Zile nyakati za sitaki uimbe mpaka ufike chuo kikuu,au sitaki ucheze mpira mpaka ufike chuo kikuu zimepitwa na wakati, mbadiliahe kijana leo ili aweze kukabiliana na hali halisi atakayokutana nayo kesho,

Kipindi ushindani umekuwa mkubwa sana, tofauti na kipindi cha nyuma tuwaeleze kizazi kijacho kuwa kuna ushindani kwenye kile hatua degree zimekuwa nyingi mpaka mtu kujitambulisha anaona aibu, tuwaeleze kizazi kijacho wawaze zaidi kuzalisha na kufanya vitu vyao binafsi na si kusubiria kazi, tuwaeleze kuwa
 
Upvote 0
Back
Top Bottom