Sio kwamba tumetulia. Watu wana hamu ya kugoma ila tatizo wanahitaji 'starter'. Nani ajitoe mhanga? Kwanza watu sasa hivi wanalifaidi boom tu, wameshasahau.
Mimi nasikitika kwa wale waliokamatwa maana hawakutendewa haki, TBC walitangaza katika habari yao saa 2 juzi kuwa wamefukuzwa kwa sababu waliharibu mali za umma, waliwapiga watu watano, wakaharibu kantini na mabasi matatu. Nashindwa kuelewa, maana hawa watu 51 hakuna ushahidi kuwa walikuwepo siku ya vurugu ya jumatatu usiku. Sasa mbona wao ndio wapewe adhabu? Wale waliofanya fujo j3 ndio wameharibu maana walikuwa wanafanya fujo sana. Mfano kuwachapa wanafunzi wenzao.