Kama ameliona hilo la siasa bungeni naomba awakanye wabunge wake wote,kuanzia spika na wengine wote.Bunge si sehemu ya siasa ingawa waliopo ni wanasiasa,kazi ya bunge ni kutunga sheria na kusimamia shughuli za serikali.wabunge hawa ndiyo wliotufikisha hapa tulipo kwa kutokujua kazi yao na kuingiza siasa ndani ya bunge.Kama spika na naib wake wangekuwa wanajua vizuri majukumu ya bunge,hakika kusingekuwa na mtu maarufu,kwa sababu wangefuata maadili ya bunge na wala si mipasho na matusi ambayo tumekuwa tukiyashuhudia kupitia hawa viongozi wa bunge.Na sijui kwanini waliamua kujiita WAHESHIMIWA? Labda niwaulize wana jf je kuna wabunge ama mawaziri wanaojiheshimu wawapo Bungeni? Je;ni nini maana ya kujiita mheshimiwa wakati huo hujiheshimu?Bunge limepoteza maadili kulirudisha mahali pake linahitaji Spika mwenye kusimamia maadili ya bunge asiyeyumbishwa na upande wowote ule.