Hatuna nia ya dhati kukabiliana na COVID-19

Hatuna nia ya dhati kukabiliana na COVID-19

Jensen salamone

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2019
Posts
320
Reaction score
641
Asubuhi na mapema leo Serikali imesitisha mbio za mwenge mwaka huu 2020 kama moja ya strategy za kukabiliana na ugonjwa wa Corona, COVID-19. Nakubaliana na uamuzi huo lakini hatujajipanga!

Tumesitisha mbio za mwenge ila mipaka ya nchi ipo wazi kuruhusu wageni kuingia na kutoka!

Kama hiyo haitoshi bado serikali imeruhusu mikusanyiko mingine kuendelea mfano halisi ni mamia ya watu walio hudhuria pale ubungo interchange kumsikiliza mh. Rais.

Mbali na hilo mikusanyiko mingine inafanyika kwenye taasisi za umma kama vile mashule, makanisa n.k

Je, tumedhamiria kweli kukabiliana na virusi vya Corona AU hatuna hela za kugharamia mbio za mwenge mwaka huu?

Kupigwa marufuku mbio za mwenge linaweza kuwa mwendelezo mwa mambo mengi yatakayositishwa huu mwaka

Mengine ni kusitisha nyongeza ya mishahara kwa wafanya kazi, ajira mpya n.k shida si COVID-19 bali kukusanya pesa kwaajili ya uchaguzi mkuu unaotegemewa kufanyika october.

Endapo hela isipopatikana basi uchaguzi utakuwa postponed kwa kisingizio cha corona kama walivyopiga marufuku ya mbio za mwenge? Muda utasema!!
 
Ukitaka kujua kwamba hatujajipanga nenda kwenye mipaka yetu. Leo hii nimetoka kuzungumza na watu waliotokea Nairobi. Nikawauliza vipi hapo Namanga. Walichoniambia nimeshindwa kuzuia hofu yangu. Ni kwamba hakuna cha kupima joto, wamepita na kugongesha passport na kuingia Tanzania.

Hii imenikumbusha wakati wa ebola, Nilikuwa nakaa nchi yenye Ebola, nilipofika Airport baada ya kupitia viwanja vilivyo serious kama Accra, Addis Ababa, sasa kilichowaponza nilipofika Nairobi nikabadilisha ndge na kupanda inayotokea Nairobi. Kumbe hawakujua kuna watu tulikuwa tunatokea Guinea, Sierra Leone na Liberia.

Kwa mbwembwe mabwana na mabibi afya wakatupima joto, wakatupa form tukajaza. Form kuna mahali wanasema kama umetokea nchi yenye ebola. Tukajaza tumetoka uko na kuweka simu zetu za contacs. Mfanyakazi alizikusanya zote bila kuangalia na tukapita. Nilitegemea watanipigia simu au mmoja wetu lakini hakuna kilichotokea. Kwa hiyo mimi naona bado kabisa hatuko serious
 
Ukitaka kujua kwamba hatujajipanga nenda kwenye mipaka yetu. Leo hii nimetoka kuzungumza na watu waliotokea Nairobi. Nikawauliza vipi hapo Namanga. Walichoniambia nimeshindwa kuzuia hofu yangu. Ni kwamba hakuna cha kupima joto, wamepita na kugongesha passport na kuingia Tanzania. Hii imenikumbusha wakati wa ebola, Nilikuwa nakaa nchi yenye Ebola, nilipofika Airport baada ya kupitia viwanja vilivyo serious kama Accra, Addis Ababa, sasa kilichowaponza nilipofika Nairobi nikabadilisha ndge na kupanda inayotokea Nairobi. Kumbe hawakujua kuna watu tulikuwa tunatokea Guinea, Sierra Leone na Liberia. Kwa mbwembwe mabwana na mabibi afya wakatupima joto, wakatupa form tukajaza. Form kuna mahali wanasema kama umetokea nchi yenye ebola. Tukajaza tumetoka uko na kuweka simu zetu za contacs. Mfanyakazi alizikusanya zote bila kuangalia na tukapita. Nilitegemea watanipigia simu au mmoja wetu lakini hakuna kilichotokea. Kwa hiyo mimi naona bado kabisa hatuko serious
Infact bado hatujajipanga kukabiliana na corona
Matamko yanayotolewa kama njia ya kujikinga na corona kwa mfano hili la marufuku ya mbio za mwenge ni siasa tu imetumika usikute serikali haina hela ila inatumia corona kama kisingizio. Right kweli tungekuwa tumedhamiria kuzuia corona isiingie tungeanza kufunga mipaka kwanza na kupiga marufuku mikusanyiko yoyote ile inayoweza kupelekea maambukizi ya hivi virusi
 
Back
Top Bottom