Hatuna viongozi wenye maono makubwa kwa Tanzania yetu

Hatuna viongozi wenye maono makubwa kwa Tanzania yetu

12STONE

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
1,189
Reaction score
407
Kwa dhamira njema kabisa, nina shauku kubwa sana kuona timu yetu ya mpira wa miguu, yaani Taifa Stars, inaenda ama kufuzu kucheza Kombe la Dunia.

Lakini sera mbovu za serikali ya chama tawala CCM, ikiwa ni pamoja na kukosa mikakati karibu kila kona ya wizara na idara, zimesababisha kudumaa kwa ustawi wa taifa letu.

Ubovu, ukongwe, na udhaifu mkubwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) vimechangia sana nchi yetu kudumaa kimichezo kwa nyanja zote, hasa soka (mpira wa miguu kwa wanaume na wanawake), riadha, na ngumi, n.k.

Kusema ukweli, CCM kama ni gari, ndege, au chombo chochote cha usafiri, kimeishiwa petroli, dizeli, au gesi. CCM haina hata mbinu mbadala za kujenga taifa letu. Miaka 63 ya uhuru wa taifa letu hatuna hata shule za michezo? Mnawaza siasa tu na siasa zenyewe mlizonazo CCM hazina mpango wa kumwinua mwananchi mmoja mmoja kiuchumi.

CCM kwenye michezo holaa; kilimo bure kabisa; elimu, mpango wa kuinua wajinga wengi wasio na uwezo wa kujiendeleza wenyewe; hospitalini, mpaka leo, mama wajawazito wanalipishwa pesa wakati wa kujifungua.

Usimamizi wa serikali ni mbovu kweli kweli. Lenu ni moja tu; mnalenga kuweka na kuendeleza watoto wenu na kikundi cha walafi wachache kujinufaisha na rasilimali zetu.

Nina shauku ya kuiona Tanzania mpya yenye viongozi wenye maono na wazalendo wa kweli wasio na unafiki, wenye kushibisha matumbo yao tu.

Pamoja na ubovu wa timu yetu ya taifa, yaani Taifa Stars, natamani iende Kombe la Dunia hata ikitokea tukanyeshewa magoli mengi. Yamkini tukapata rais mpya na chama kingine kitakachoweka mabadiliko ya kudumu kwenye michezo na Tanzania yetu ikapata heshima mbele ya mataifa yote.
 
Back
Top Bottom