Hatupaswi kulipa Uingereza kwa mkataba uliovunjwa - Rwanda

Hatupaswi kulipa Uingereza kwa mkataba uliovunjwa - Rwanda

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Hatupaswi kulipa Uingereza kwa mkataba uliovunjwa - Rwanda
.


Rwanda imesema haitakiwi kuirudishia Uingereza pesa baada ya makubaliano ya mamilioni ya pauni ya wahamiaji kati ya nchi hizo mbili kufutiliwa mbali.

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza na kiongozi wa Chama cha Leba Keir Starmer alitangaza mwishoni mwa juma kwamba mpango wa kuwafukuza baadhi ya watu wanaotafuta hifadhi nchini Rwanda "umekufa na kuzikwa".
Mpango huo ulibuniwa na serikali ya awali ya Conservative, ambayo tangu kuuzindua mwaka 2022 imelipa Rwanda £240m ($310m).

Uamuzi wa kisheria ulimaanisha kuwa mpango huo haujaanza na Uingereza ilionyesha matumaini Jumatatu kwamba pesa kutoka kwa mpango huo zinaweza kurejeshwa.

Siku iliyofuata, msemaji wa serikali ya Rwanda aliiambia televisheni ya taifa ya nchi hiyo: "Jambo hili lieleweke wazi, kulipa pesa hakukuwa sehemu ya makubaliano."

Alain Mukuralinda alisema mkataba huo "haujaweka wazi" pesa zinapaswa kurejeshwa na kwamba Uingereza iliwasiliana na Rwanda na kuomba ushirikiano, ambao "ulijadiliwa kwa kina".

Mnamo mwezi Januari, baada ya miezi 21 ya mpango huo kukwama, Rais wa Rwanda Paul Kagame alipendekeza pesa zingine zingeweza kurejeshwa ikiwa hakuna waomba hifadhi waliotumwa nchini humo.

Lakini serikali ya Rwanda baadaye ilisema "sio wajibu" kurejesha pesa kwa Uingereza.

Waziri Mkuu Starmer aliutaja mpango huo kuwa "ujanja" baada ya Chama cha Labour kushinda uchaguzi kwa kishindo wiki iliyopita.

Chama chake kimeahidi badala yake kuunda Kamandi mpya ya Usalama Mipakani ili kukabiliana na magenge yanayosafirisha watu.

Upinzani dhidi ya mswada huo pia ulitoka pande nyingine - Mahakama ya Juu Zaidi ya Uingereza ilipoamua mpango huo kuwa kinyume cha sheria, mashirika ya haki za binadamu yaliutaja kuwa ni wa kikatili na wa kibabe, huku wapinzani ndani ya Chama cha Conservative wakishinikiza kufanyiwa marekebisho ambayo yangeulinda vyema mpango huo dhidi ya pingamizi za kisheria.

Serikali iliyopita ilisema mpango huo ulilenga kuwazuia watu kuvuka Mlango-Bahari wa Uingereza kwa boti ndogo.
Uhamiaji haramu ni mojawapo ya changamoto kuu zinazoikabili serikali ya Uingereza. chanzo BBC.
 
Hahahaha! Hiyo nzuri. Halafu Kagame huwa anatazama ya mbele. Huu mkataba ina maama kama wangeenda pale Rwanda wakajaa kwa sababu ardhi ni ndogo, Kagame hata angewasukumia nchi jirani
kwani hakuna kipengele kinachowalazimu uingereza kuwalipa rwanda kwa kuvunja mkataba?
 
Back
Top Bottom