Hatutaki viwanda vinavyotugeuza watumwa na mateka wa nchi yetu wenyewe

Mkuu RH kwanza kongole,kwa mada ya kuelimisha,funzo na muono wa mbali.Hawa matajili wenye asili ya Asia,wamewafanya waafrika kuwa watumwa kwenye Viwanda visivyo na mazingira rafiki ya kufanyia Kazi.Na mbaya zaidi viongozi wetu wanalifahamu vema jambo hili.

Ugumu wa kuchukua maamuzi unakuwa mgumu sababu hao hao ndo watoa pesa za kugharamia kampeni zao.
 
Watanzania wengi ni mateka wa chama dola kongwe uwe kibarua, mkulima, bodaboda, daktari, mwalimu n.k

CCM ukichagua wao tayari wanajua mmekubali kuwa mateka wao, maana hakuna vyama huru vya wafanyakazi manamba, waalimu, wafanyakazi wa viwandani, bandarini wala vyama huru vya ushirika wa wakulima n.k

Hivyo vyama vya wafanyakazi, taaluma n.k ni jumuiya mojawapo nyingi za CCM kama UVCCM, WAZAZI, BAKWATA n.k
 
Nashukuru mkuu kwa uchambuzi murua kabisa juu ya kadhia wanatipata vijana wenzetu
INGAwa nimeiona late
Mimi pia niliwahi kufanya kazi kwenye viwanda pia Tena Cha Nguo kwa wahindi
Na Wakati nilikuwa kitengo Cha kuchanganya Yale machemical ya na rangi za Nguo
Na mshahara ulikuwa haifiki hata elfu tano kwa siku

So nafahamu Changamoto za viwandani

Lakini Cha kushangaza na ambacho ndo point yangu ni kwamba maelfu ya vijana wanapambana kupata hizo nafasi
Na hupati kirahisi lazima uwe na connection Kali
Na ukicheza wahindi wanaweza kukuzibua mabanzi saa yoyote 🙄🙄
Au ufukuzwe kazi
So swali la kujiuliza ni kwanini kazi Kama vijana wanapambana kuzipata hata kwa rushwa wakati mwingine

Tukijua sababu ya vijana kujipeleka utumwani wenyewe bila kulazimishwa
 
Ka
Kabla ya kuwalauma waajiri wa viwanda
Tujiulize kwanini vijana wenzetu wanajipeleka wenyewe Tena kwa kupambana ili kufanya hizo kazi mnazoita za kitumwa
 
Kuandika tu inafaa ? Andika na peleka bungeni peleka barua kwa Rais tume zoote uwekezaji etc .....wamejisahau kuacha sekta binafsi kuamua hizo posho sijyi wizara kama ina policy za bei elejezi wanyonge wanateseka mno hakuna wa kuwasemea....wizara wanalipana posho kwenda kulagua ujinga vitu muhimu hawagusi kama maslahi ya wafanyakazi
 
Mradi tupo kwenye bangi system ya kimataifa na tunaendeelea kuwa na hadhi ya kukopesheka, tutaendelea kuwa watumwa daima.

Kuondokana na utumwa ni kuibadili hadhi yetu na kuwa na hadhi ya kukopesha.
 
"Lakini Cha kushangaza na ambacho ndo point yangu ni kwamba maelfu ya vijana wanapambana kupata hizo nafasi
Na hupati kirahisi lazima uwe na connection Kali
Na ukicheza wahindi wanaweza kukuzibua mabanzi saa yoyote [emoji849][emoji849]
Au ufukuzwe kazi
So swali la kujiuliza ni kwanini kazi Kama vijana wanapambana kuzipata hata kwa rushwa wakati mwingine

Tukijua sababu ya vijana kujipeleka utumwani wenyewe bila kulazimishwa"


UMASKINI NA KUKOSA ELIMU SAHIHI NDO SABABU
 
Mradi tupo kwenye bangi system ya kimataifa na tunaendeelea kuwa na hadhi ya kukopesheka, tutaendelea kuwa watumwa daima.

Kuondokana na utumwa ni kuibadili hadhi yetu na kuwa na hadhi ya kukopesha.

Sasa tufanyaje ili tuingie kwenye hadhi ya kukopesha?
 
Na ukipita asubuhi unakuta watu wengi wamejazana getini kupambania nafasi kwa malipo ya 5000, hapo kula, kunywa na nauli juu yako.

Nilishawahi kutana na dogo alikuwa anafanya hizo kazi za kiwandani, anakwambia ni ngumu kiasi kwamba kuna muda anazuga kwenda chooni kupumzika na kulia kidogo kupunguza machungu. Na akienda anakuta rundo la watu wamejibanza nao wanapumzikia chooni. Hapo sijui ndio mlinzi/supervisor anakuja kuwafurumusha mrudi kupiga kazi!!

Kwa kweli tunaweza kuona shetani ni mbaya kuliko, lakini binafsi naamini kama kuna kitu kibaya huku duniani basi ni umasikini uliopitiliza!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…