Hatuwezi kutumia stoku ya nchi kupunguza bei ya mafuta?

Hatuwezi kutumia stoku ya nchi kupunguza bei ya mafuta?

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
324
Reaction score
649
SERIKALI HAINA UWEZO WA KUPUNGUZA HIZI BEI ZA MAFUTA?

Na Elius Ndabila
0768239284

Nimesoma bei mpya ambazo zinaongeza maumivu mara dufu kwa mtu wa chini. Nimesema zinaongeza maumivu kwa mwananchi wa Chini kwa kuwa natambua wengine wanaotumia sawa sawa kodi za wavuja jasho maumivu hayawafikii kisawasawa.

Bei ya mafuta iliyotangazwa leo lita Moja kwa Ileje itanunuliwa 3,381/=. Yaani ukiwa na 10,000/= ambayo ulikuwa unanunua Lita 5 , sasa utanunua lita 2.

Tafsiri yake ni kuwa asilimia kubwa ya vitu tunavyotumia ndani navyo vitapanda bei. Kwa mfano Chumvi, sukari, Sabuni, Saruji, Mafuta n.k vyote vitapanda bei. Hapa namba tutaisoma zaidi sisi tunaokula Kwa jasho letu, wanaokula Kwa jasho letu maumivi siyo makubwa.

Mwezi January niliwahi kuandika ili kuweza kukabiliana na changamoto ya hizi za bei serikali ingeweza kustisha baadhi ya miradi mipya mikubwa Kwa muda ili kumsaidia mwananchi wa chini. Lakini bahati mbaya machozi ya samaki yanaishia majini. Lakini ukweli hili lingefanyika bei hii isingefika huku kwa kuwa kuna tozo serikali ingeziondoka kwenye mafuta ili kupunguza mfumuko huu.

Vita hii ya uchumi, kila Taifa linapaswa kukabiliana nayo kwa namna linavyoona inafaa. Hatuna sababu ya kukopi mbinu za kivita kuwasaidia wananchi wetu.

Swali lingine ninalojiuliza ni kuwa tuliambiwa nchi ina stock ya mafuta. Sasa haya mafuta yanafanya nini kwenye stoku, Kwa nini yastolewe kuja kupunguza gharama hizi? Au nayo yanauzwa Kwa Tshs3,381/=?

Wabunge nyie ndio silaha pekee iliyobaki kuwatetea Wananchi na kuishauri serikali namna nzuri ya kukabiliana na changamoto hii. Kuna faida gani kujivunia kijenga miradi mikubwa inayotumia fedha nyingi kama unaowajengea hawanafuraha moyoni? Kuna faida gani kujivuna kujenga miradi mikubwa kama unaowajengea hawajui mchana wanakula nini? Tuanze kuwatengenezea kwanza furaha watu ndipo tuingie kwenye uwekezaji.

Furaha ya Wananchi ni kuona wanamudu bei ya vitu sokoni, wanamudu nauli za usafiri hapo ndipo wataongeza amani ya moyo. Mfumko huu usipodhibitiwa, tunaenda kuongeza wagonjwa wa vidonda vya tumbo, presha na magonjwa ya akili yanayosababishwa na msongo wa mawazo.
 
Mie Naiwaza Ile Tozo Ya 'Uzalendo' Ya Miamala Ya Simu...hivi inaenda Wapi Mama..? Huwezi Kuturudishia Kwa njia ya Ku subsidize Mafuta? Sasa hali Mafuta inang'ata ....!
 
Hiyo stock watu wanayoisemea iko wap?..Magufuli ndio alitaka kujenga storage ya mafuta ya serikali
 
Hhaahahahahaha wenye vyombo vya moto naona imepenya hii sasa hili swala tuendelee kuvumiliana tu serikali haina kisima cha mafuta
 
Stoku?

Kuna siku Makamba eti anajivuna mbele ya wabunge, hoo yuna mafuta yakutosha kwa muda wa wiki 3 hata meli isipokuja kabisa!

Upumbavu mtupu
 
Ipo siku mafuta yatakuwa hakuna kabisa, ndipo tutaimba pamoja wimbo wa ... lala salama huko uliko mzalendo halisi.....
 
Nimefurahia kamsemo eti. "machozi ya samaki huishia majini"

saikolojia ya Watanzania nyepesi sana. Kelele sana na baadae maisha yanaendelea na mwezi ujao bei itapanda. Hutaki neda kaishi BURUNDI.
 
Viongozi wamefundishwa kuwapuuza watanzania

Hii ni kutokana na kulalamika kwenye kila kitu
 
Back
Top Bottom