Haujengi kwenye kiwanja chako kwa sababu uliyemkabidhi akulindie kakichezea

Haujengi kwenye kiwanja chako kwa sababu uliyemkabidhi akulindie kakichezea

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Haya maono niliyapata kitambo sana ila leo nimeamua kuyawasilisha.

Watu wengi wana mtindo wa kununua maeneo halafu wanatafuta mwenyeji wa pale wanamkabidhi awalindie. Wanamruhusu "mlinzi wao" alime na kinachopatikana achukue.

Kinachotokea yule unayemkabidhi ananogewa na fursa ya kulima na kufanya biashara katika kiwanja na shamba lako na hatataka uje upaendeleze halafu yeye apoteze fursa hiyo.

Anachofanya mlinzi wako ni kuchezea udongo wa kiwanja au shamba lako. Miaka 3 inakuwa 6, miaka 6 inakuwa 15, hata msingi haujajenga na kukiuza haukiuzi. Unapambana wee inafika wakati hata mawazo ya kujenga pale au kufanya kilimo cha maana yanayeyuka.

USHAURI: Tenga siku moja nenda katika kiwanja au shamba lako ambalo muda mrefu umeshindwa kupaendeleza. Anza kutembea kwenye mipaka yake, kona moja hadi nyingine huku ukiomba na kunena mambo unayotaka kufanya pale. Nenda pia maeneo ya katikati. Fanya hivyo huku ukiwa unachota na kutembea na udongo wa eneo lako. Fanya hayo kwa utulivu bila kubughudhiwa na mtu yoyote ikiwemo na mlinzi wako.

Ikiwezekana mwambie mlinzi wako utamlipa mshahara kama ulikuwa haufanyi hivyo ila usimruhusu afanye biashara yoyote katika eneo lako. Fyeka na safisha eneo lako, mwambie unaenda kuanza ujenzi hivi karibuni.
 
Ni kweli...hata hao wanaotulindia nyumba zetu ndio tabia zao.
Kuna kanisa walikodisha jengo/nyumba ya mzee wetu,kila akiwaambia waondoke anahitaji aitumie,walikuwa wanasali na kufunga mzee asiwaondoe.
 
Ni kweli...hata hao wanaotulindia nyumba zetu ndio tabia zao.
Kuna kanisa walikodisha jengo/nyumba ya mzee wetu,kila akiwaambia waondoke anahitaji aitumie,walikuwa wanasali na kufunga mzee asiwaondoe.
Wewe umenielewa.
 
Back
Top Bottom