Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
HAUPO ULIVYO! DUNIA HAIPO ILIVYO!
Mpaka miaka mitano iliyopita sikuwa naamini katika mambo ya kiroho, niliamini katika elimu yangu,na bahati mbaya nilikua nimesomea mambo ya sayansi katika miaka yangu yote ya sekondari(kidato I-VI)hivyo niliamini sana katika elimu, sayansi na teknolojia,wakati fulani baada ya kusoma kitabu kilichoandikwa na Warusi wakomunist kinaitwa THE DIALECTICS OF MATERIALISM (sikumbuki mwandishi) nilishawishiwa juu ya elimu ya maumbile yaani Physical Science ambayo ndiyo msingi wa uwepo wa imani inaitwa ATHEISM.
Atheism ambayo wafuasi wake wanaitwa Atheists inaamini katika misingi ya unyambuzi wa kinasaba(evolution) kuwa ndiyo msingi wa uwepo wa vitu vyote, haiamini katika uumbaji hivyo kwao HAKUNA MUNGU!
Niliponea chupuchupu kuwa ATHEIST!!
Kuanzia mwaka 2014 ndipo nilipoanza kupata uvuvio wa kuona dunia ya kiroho nje ya mwili, mengi ya uharibifu yalifuata lakini katika hayo ndipo nilipojua kuwa mwanadamu na maisha yake anazungukwa na anaishi katika roho sawa na anavyoishi katika mwili!
Kati ya 2014 mpaka leo nimekutana na mengi magumu lakini yaliyonifunulia zaidi kuhusu ulimwengu wa roho, kwa sasa ninaweza kuandika makala ama kitabu juu yake!
Ukimsimulia mtu wakati mwingine unaonekana kama mwehu ama mshirikina, unaamua kukaa kimya!!
Lakini Mungu akujalie kuuona ulimwengu wa kiroho utajifunza mengi na sana utajifunza kuwa mnyenyekevu na kujifunza na kumtii Mungu!
Kutoka hapo hautawatazama wanadamu na dunia hii kama wanavyoonekana (inavyoonekana)! Kuna dunia zaidi ya hii unayoijua, muombe Mungu akufunulie!🤔🤔🤔🤔
Nsaji Mwasege