Jamani mimi natoka kusini na bahati mzuri nimefanya kazi na Hawa Ghasia katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi akiwa kama Afisa Mipango wetu wa Wilaya.
Ukweli ni kuwa hawa ni watu wawili tfauti na hawana unasaba wowote,sijui tatizo Mama Kikwete kuwa mtu wa Lindi na Hawa Ghasia kutoka kusini.
Hawa Ghasia ni mwenyeji wa Mtwara vijijini na Salma Kikwete ni mwenyeji wa Lindi mjini.Pamoja na tofauti hizi kubwa ni kuwa Hawa Ghasiaanatoka ktk familia za kimakonde wa bara na Salma yaonekana na mchanganyiko na makabila mengine lakini ni mmakonde wa pwani(wamalaba).Ata mume wa Ghasia ambaye ni Yahya hana nasaba zozote na hawa watu hivyo si sahihi kusema kuwa amebakishwa kwa maslahi ya Kikwete.Na chakujiuliza ni kuwa Utumishi kuna maslahi gani pale?Mama Nagu mpaka anamaliza maekuwa na kashfa pale,kama wangetaka alinde maslahi yao nadhani wangempeleka madini,Hazina,Maliasili hizi ndizo sehemu ambazo kwakweli Mawaziri wanaweza kulinda maslah.
Kikwete amemweka yule mama ni kwasababu mara nyingi ktk Utumishi wa Umma serikali za Mitaa wamekuwa wakitupwa nyuma sasa uwepo wa Ghasia pale ni mzuri ukilinganisha ana uzoefu wa kutosha wa serikali za mitaa na alikuwa Afisa mipango wetu Bomba tu.
Na kilichamvutia Kikwete ni kuwa huyu mama amepata Ubunge jimboni kwa kumwangusha mbunge anayetetea jimbo sio viti maalumu.
Sifa anazo na anastahiki kuwa Waziri.
NI UZUSHI MTUPU KUSEMA HAWA GHASIA NA SALMA KIKWETE WANAUDUGU WOWOTE. Nadhani tujadili mambo ya uhakika na si kuja na tetesi kama hizi kwakuwa hawa wote ni wa kusini.