Hawa hapa Wabunge wapya watakaoiwakilisha Tanzania EALA

Hawa wawe tofauti na kina Kimbisa, Makongoro maana wabunge wa EALA toka Uganda, Kenya na Rwanda tunawasikia wakichangia hoja lakini wetu wa kutoka Tanzania wamekuwa mabubu .
Lugha ya Malkia ngumu ilikuja na British Airways🥰🥰🥰
 
Hujazidiwa sifa, sema hawakuwataka tu nyie
Ina maana kizigha anaweza kukuzidi sifa
Nlikuambia tangu mwanzo mfumo wetu unataka watu akili ndogo ndiyo ziwe zinatuwakilisha....

Ova
Kwenye wale 8 wa CCM, kuna Ph.D 3, daktari wa medicine 1, wanne waliobaki wote wana masters mbili mbili!.
Kiukweli kabisa nimezidiwa sifa na vigezo.
P
 
Nina kila sababu ya kuiombea CCM inyimwe kura 2025 na kuendelea.

Haya majina yanaashiria utawala wa kisultani ndani ya CCM unavyoenda kuiathiri nchi.
 
Kwenye wale 8 wa CCM, kuna Ph.D 3, daktari wa medicine 1, wanne waliobaki wote wana masters mbili mbili!.
Kiukweli kabisa nimezidiwa sifa na vigezo.
P
Mkuu Pasco.
Uongozi siyo wingi wa vyeti bali ni dhamana inayohitaji Hekima, Busara na Elimu. Bora ukose usomi lakini hekima na busara ukawa navyo. Lakini ukiwa na Elimu bila Hekima na Busara ndo tunapata aina ya maongozi ya kuhamasisha wananchi waende Burundi kama.jibu la malalamiko yao.

Ninachokiona hapo ni impact ya siasa za Kisultani ndani ya CCM inavyoenda kuoathiri nchi
 
Kizigha, Maghembe na Ansar hao NI kama wanaendelea tu nyadhifa zao siyo wageni na Bunge la EALA
 
Ansar yupo vizuri nilihudhuria kongamano moja UD yeye aliongea alionyesha yupo vizuri kichwani
Ansar kachwamba aliwahi kua headmaster wangu jamaa yupo vizuri hataki masikhara kabisaaa
 
Kafanyaje mwalimu wetu?
 
Mkuu unamfahamu baba yake na KCU(chama cha ushirika cha wakulima mkoani Kagera) CCM, Shule za sekondari za wakulima, nk?
Kusema ukweli m sijui maisha ya kwao mimi alikua headmaster wangu ndo namfahamu ivo tu
 
CCM haitegemei mtazamo wa wapiga kura, shtuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…