SoC03 Hawa hawana Umungu wowote

SoC03 Hawa hawana Umungu wowote

Stories of Change - 2023 Competition

Gill Rugo

Member
Joined
Aug 28, 2022
Posts
30
Reaction score
121
Kuna ukakasi fulani kuhusu matumaini; yanakufanya uamini utamu unaowezekana- ikiwa tu uking’ang’ania zaidi- kabla hujavunjika moyo. Kisha yanachipua tena, na muda huu- kama tochi yenye betri jipya. Halafu tena, haiwi kama ulivyotegemea, au labda wakati huu inakua kama yalivyosema. Lakini ningefanya nini zaidi ya kuyashikilia? Na nizishukuru mbingu, japo ni kwa sekunde tu lakini nahisi nitatoboa. Halafu yananiponyoka tena, kama hayakuwahi kuwa yangu vile.

Nina uhakika hakuna anayejali. Kwa namna yao, watakuwa wameweza kuyafanya mateso yangu kuwa kichekesho. Wapo watakaosema nasitahili kinachonikuta, wengine watakua wakihoji ningepungukiwa nini kama ningekaa kimya, na najua yupo atayevumisha nimelatiwa. Na kusema ukweli, sikumbuki kama haikuwa hivyo. Najua kwanini wapo hivyo- inahusisha zaidi ukweli wa kwamba wanapata faraja kujua kuna mtu anapitia magumu zaidi kuliko wao, na pia ni wanyonge wasio na nguvu ya kufanya kitu tofauti na kujificha nyumba ya kibodi.

Nilipoteza fahamu wakati narudi nyumbani. Sijui jinsi ilivyotokea na kusema kweli, haijalishi tena. Ni sababu ndiyo niliyotamani kujua pale mnyunyizo wa maji baridi uliponiamsha. Kabla hata sijakaa sawa, rungu la kichwa lilinirudisha kwenye ulimwengu niliotoka. Ilikua hivyo kwa muda ambao wanajua wao tu; nikiamshwa ili tu nipigwe tena mpaka nizimie. Ili kujilinda, mwili wangu ulikufa ganzi, lakini jambo moja lilikua dhahiri- serikali yangu ilikuwa ikiniadhibu kwa kuthubutu kuiomba uwajibikaji.

Unaona, asubuhi yake nilishiriki kwenye maandamano ya kupinga ukatili wa polisi. Ilibidi tuanzie Cape Town, tupige mchakamchaka mpaka Kinshansha kabla ya kupumzika kidogo pale Kampala. Halafu safari ya kuitafuta Cairo ingeanza baada ya kupata neno la matumaini pale Lagos. Nakumbuka nilikuwa wa saba na wa mwisho kufika. Baada ya kilele cha mchana, ikawa wazi kwamba- licha ya mamilioni ya machangio kwenye uzi wetu wa Twitter, na ahadi za kutokea tulizopata Facebook- hakuna mwingine anayekuja.

Kwahiyo tukaliamsha. Tuliimba. Tukanyanyua mabango. Tukapaza sauti. Na, yote hayo tukiyafanya kwa tarajio la wengine kujiunga nasi.

Hakuna hata mmoja aliyeongezeka.

Kipindi nateswa niliwaza sana. Kwa sababu unamkimbilia nani pale serikali yako inapotaka kukuua? Nikaamua kulikimbilia kimbilio la wanyonge. Nafsini nikaiangalia mbingu na kumuita yule mwenye nguvu kiasi cha wafalme kumsujudia.

Lakini subiri! Katikati ya sala yangu, jambo fulani linanigonga…

Si ni Mungu ndiye wanajaribu kumuiga? Mungu ndiye mfano wao wa kuigwa. Mda wote huu, serikali yangu imekua ikijaribu kucheza nafasi ya Mungu!

Miaka 30 iliyopita, wazazi wa watawala wetu walimwaga damu zao kwa ajili ya uhuru wa bara letu , na kwa sababu hiyo- watawala wanahisi hili bara ni la kwao. Ni kana kwamba sadaka za mababu zetu sisi kipindi cha MAUMAU hazihesabiki! Ni kana kwamba wamesahau kuwa hata sisi mabibi zetu walibakwa na mkoloni!

Nafahamu dhahiri kwamba mbinguni ni udikteta. Chochote anachotaka Mwenyezi Mungu ndicho huwa. Kama akitaka kuiloweka dunia nzima kwenye maji basi malaika wataikimbilia nafasi ya kuzifungua koki. Kama akitaka kunyang'anya nchi kutoka kwa taifa moja na kulipa taifa lingine basi malaika wataenda kuziangusha kuta za miji ya adui. Haijalishi jambo linaukatili kiasi gani, linafanywa kwa ajili ya manufaa makubwa zaidi. Na hivyo pia, ndivyo serikali yangu ilivyo.

Ili kuwa waweza yote, wametengeneza jeshi lenye nguvu na kujitikwa dhazifa zote. Vivo hivyo pia wamefanya kwa polisi na mahakama, kwa bunge na vyama siasa- hata vile vya upinzani. Hakuna jambo linalofanyika bila idhini yao. Na kibaya zaidi ni kwamba huwezi kumuuliza waziri wa ulinzi kwa nini ametumia bajeti ya wizara kwa matumizi yake binafsi kama ambavyo huwezi kumuuliza Mungu kwanini aliwaruhusu watoto wachanga wafe pale Sodoma.

Ili kuwa kila mahali, wametunga sheria nyingi, nyingine zisizo na msingi wowote na kuzisindikiza na vituo vya ukaguzi kila mahali. Na pale unapofikiri hawapo, hapo ndipo wameweka mtandao wa majasusi ili wayajue yote, ikiwemo na yale tunayofikiria. Wanajifanya madaktari, wao ndio mainjinia, wanakuwa wachambuzi, na wanafanya yote kwa ustadi unaoweza kumfanya mtu aamini kweli wanajua wote- lakini ukweli ni kwamba wametunyima elimu bora ya kutufanya tuone mapungufu ya mfumo wao.

Ili kuwa wasio na mwisho, wameweka mfumo duni wa uchaguzi ambao huruhusu udanganyifu. Mfumo ambao mabadiliko ya madaraka ni kwa matakwa yao na sio matakwa ya wananchi. Pia, uongozi wanapewa wale waliotayari kupeperusha propaganda zao, na wale wa familia zao. Ndiyo maana vyeo hupitishwa kulingana na ukabila na familia; ili tu kama, watawala wakifa basi watoto wao warithi bara.

Ili kuwa wakamilifu, sheria wameandika wao. Wao pekee ndio wanachagua lipi ni baya na lipi ni zuri. Wamevifanya vitabu vitakatifu kuwa msingi wa sheria zao. Na kwa misingi hiyo, wanasafisha jinai zao: kwamba zimefanywa ili kulinda usalama wa taifa. Ni kwa misingi hiyo hiyo pia wanawaaminisha raia kwamba hawawezi kudanganya, na hivyo yeyote mwenye maoni tofauti na yao ni adui.

Nilipolala ni kingoni mwa mto walionitupa. Kiungo pekee kinachoweza kusogeza ni macho. Na kinatosha kuwaona jinsi walivyo: wameshindwa, wameliangusha bara letu, hawako na ujuzi wa kila kitu; vinginevyo, kwa nini hatuna maji baada ya miaka 30? hawana nguvu yoyote; nguvu ya kweli ni wananchi, hawana ukamilifu; wanatishia ili kushikilia dola.

Na juu ya yote hawana upendo. Wameshindwa kuvienzi vita vya uhuru wa Afrika.

Baada ya kuridhia hatima yangu, ninafumba macho kukingoja kifo. Lakini naona kitu, mwanga ukijongea kwangu. Kisha taa zaidi, halafu msindo mkali wa nyimbo unafuata. Ni watu wengi wanaoimba, na nyimbo hii naifahamu fikra. Ni nyimbo ile ile aliyoimba Mandela akiwa gerezani, ni nyimbo ile ile aliyoimba Lumumba kabla ya kupigwa risasi.

Mara ghafla! Tumaini jipya linaning'ata: Leo sio siku ya kufa, bado kuna kijana inabidi tumtoe nyuma ya kibodi, tuandamane nae kuwawajibisha hawa. Kazi ya mababu zao haiwapi hati miliki ya bara letu la Afrika.
 
Upvote 18
Kuna ukakasi fulani kuhusu matumaini; yanakufanya uamini utamu unaowezekana- ikiwa tu uking’ang’ania zaidi- kabla hujavunjika moyo. Kisha yanachipua tena, na muda huu- kama tochi yenye betri jipya. Halafu tena, haiwi kama ulivyotegemea, au labda wakati huu inakua kama yalivyosema. Lakini ningefanya nini zaidi ya kuyashikilia? Na nizishukuru mbingu, japo ni kwa sekunde tu lakini nahisi nitatoboa. Halafu yananiponyoka tena, kama hayakuwahi kuwa yangu vile.

Nina uhakika hakuna anayejali. Kwa namna yao, watakuwa wameweza kuyafanya mateso yangu kuwa kichekesho. Wapo watakaosema nasitahili kinachonikuta, wengine watakua wakihoji ningepungukiwa nini kama ningekaa kimya, na najua yupo atayevumisha nimelatiwa. Na kusema ukweli, sikumbuki kama haikuwa hivyo. Najua kwanini wapo hivyo- inahusisha zaidi ukweli wa kwamba wanapata faraja kujua kuna mtu anapitia magumu zaidi kuliko wao, na pia ni wanyonge wasio na nguvu ya kufanya kitu tofauti na kujificha nyumba ya kibodi.

Nilipoteza fahamu wakati narudi nyumbani. Sijui jinsi ilivyotokea na kusema kweli, haijalishi tena. Ni sababu ndiyo niliyotamani kujua pale mnyunyizo wa maji baridi uliponiamsha. Kabla hata sijakaa sawa, rungu la kichwa lilinirudisha kwenye ulimwengu niliotoka. Ilikua hivyo kwa muda ambao wanajua wao tu; nikiamshwa ili tu nipigwe tena mpaka nizimie. Ili kujilinda, mwili wangu ulikufa ganzi, lakini jambo moja lilikua dhahiri- serikali yangu ilikuwa ikiniadhibu kwa kuthubutu kuiomba uwajibikaji.

Unaona, asubuhi yake nilishiriki kwenye maandamano ya kupinga ukatili wa polisi. Ilibidi tuanzie Cape Town, tupige mchakamchaka mpaka Kinshansha kabla ya kupumzika kidogo pale Kampala. Halafu safari ya kuitafuta Cairo ingeanza baada ya kupata neno la matumaini pale Lagos. Nakumbuka nilikuwa wa saba na wa mwisho kufika. Baada ya kilele cha mchana, ikawa wazi kwamba- licha ya mamilioni ya machangio kwenye uzi wetu wa Twitter, na ahadi za kutokea tulizopata Facebook- hakuna mwingine anayekuja.

Kwahiyo tukaliamsha. Tuliimba. Tukanyanyua mabango. Tukapaza sauti. Na, yote hayo tukiyafanya kwa tarajio la wengine kujiunga nasi.

Hakuna hata mmoja aliyeongezeka.

Kipindi nateswa niliwaza sana. Kwa sababu unamkimbilia nani pale serikali yako inapotaka kukuua? Nikaamua kulikimbilia kimbilio la wanyonge. Nafsini nikaiangalia mbingu na kumuita yule mwenye nguvu kiasi cha wafalme kumsujudia.

Lakini subiri! Katikati ya sala yangu, jambo fulani linanigonga…

Si ni Mungu ndiye wanajaribu kumuiga? Mungu ndiye mfano wao wa kuigwa. Mda wote huu, serikali yangu imekua ikijaribu kucheza nafasi ya Mungu!

Miaka 30 iliyopita, wazazi wa watawala wetu walimwaga damu zao kwa ajili ya uhuru wa bara letu , na kwa sababu hiyo- watawala wanahisi hili bara ni la kwao. Ni kana kwamba sadaka za mababu zetu sisi kipindi cha MAUMAU hazihesabiki! Ni kana kwamba wamesahau kuwa hata sisi mabibi zetu walibakwa na mkoloni!

Nafahamu dhahiri kwamba mbinguni ni udikteta. Chochote anachotaka Mwenyezi Mungu ndicho huwa. Kama akitaka kuiloweka dunia nzima kwenye maji basi malaika wataikimbilia nafasi ya kuzifungua koki. Kama akitaka kunyang'anya nchi kutoka kwa taifa moja na kulipa taifa lingine basi malaika wataenda kuziangusha kuta za miji ya adui. Haijalishi jambo linaukatili kiasi gani, linafanywa kwa ajili ya manufaa makubwa zaidi. Na hivyo pia, ndivyo serikali yangu ilivyo.

Ili kuwa waweza yote, wametengeneza jeshi lenye nguvu na kujitikwa dhazifa zote. Vivo hivyo pia wamefanya kwa polisi na mahakama, kwa bunge na vyama siasa- hata vile vya upinzani. Hakuna jambo linalofanyika bila idhini yao. Na kibaya zaidi ni kwamba huwezi kumuuliza waziri wa ulinzi kwa nini ametumia bajeti ya wizara kwa matumizi yake binafsi kama ambavyo huwezi kumuuliza Mungu kwanini aliwaruhusu watoto wachanga wafe pale Sodoma.

Ili kuwa kila mahali, wametunga sheria nyingi, nyingine zisizo na msingi wowote na kuzisindikiza na vituo vya ukaguzi kila mahali. Na pale unapofikiri hawapo, hapo ndipo wameweka mtandao wa majasusi ili wayajue yote, ikiwemo na yale tunayofikiria. Wanajifanya madaktari, wao ndio mainjinia, wanakuwa wachambuzi, na wanafanya yote kwa ustadi unaoweza kumfanya mtu aamini kweli wanajua wote- lakini ukweli ni kwamba wametunyima elimu bora ya kutufanya tuone mapungufu ya mfumo wao.

Ili kuwa wasio na mwisho, wameweka mfumo duni wa uchaguzi ambao huruhusu udanganyifu. Mfumo ambao mabadiliko ya madaraka ni kwa matakwa yao na sio matakwa ya wananchi. Pia, uongozi wanapwewa wale wachache waliotayari kupeperusha propaganda zao, na wale wa familia zao. Ndiyo maana vyeo hupitishwa kulingana na ukabila na familia; ili tu kama, watawala wakifa basi watoto wao warithi bara.

Ili kuwa wakamilifu, sheria wameandika wao. Wao pekee ndio wanachagua lipi ni baya na lipi ni zuri. Wamevifanya vitabu vitakatifu kuwa msingi wa sheria zao. Na kwa misingi hiyo, wanasafisha jinai zao: kwamba zimefanywa ili kulinda usalama wa taifa. Ni kwa misingi hiyo hiyo pia wanawaaminisha raia kwamba hawawezi kudanganya na hivyo, yeyote mwenye maoni tofauti na yao ni adui.

Nilipolala ni kingoni mwa mto walionitupa. Kiungo pekee kinachoweza kusogeza ni macho. Na kinatosha kuwaona jinsi walivyo: wameshindwa, wameliangusha bara letu, hawako na ujuzi wa kila kitu; vinginevyo, kwa nini hatuna maji baada ya miaka 30? hawana nguvu yoyote; nguvu ya kweli ni wananchi, hawana ukamilifu; wanatishia ili kushikilia dola.

Na juu ya yote hawana upendo. Wameshindwa kuvienzi vita vya uhuru wa Afrika.

Baada ya kuridhia hatima yangu, ninafumba macho kukingoja kifo. Lakini naona kitu, mwanga ukijongea kwangu. Kisha taa zaidi, halafu msindo mkali wa nyimbo unafuata. Ni watu wengi wanaoimba, na nyimbo hii naifahamu fikra. Ni nyimbo ile ile aliyoimba Mandela akiwa gerezani, ni nyimbo ile ile aliyoimba Lumumba kabla ya kupigwa risasi.

Mara ghafla! Tumaini jipya linaning'ata: Leo sio siku ya kufa, bado kuna kijana inabidi tumtoe nyuma ya kibodi, tuandamane nae kuwawajibisha hawa. Kazi ya mababu zao haiwapi hati miliki ya bara letu la Afrika.
Nice
 
Back
Top Bottom