Hawa jamaa wanapenda sana kujisifu. Ona sasa!

Duh MaCCM mumeishiwa kweli hadi mumekimbilia kwenye taarifa za ugomvi wa wachuuzi/machinga na polisi Kenya, au mumesahau huko kwenu haya ni mambo ya kawaida...


 
Duh MaCCM mumeishiwa kweli hadi mumekimbilia kwenye taarifa za ugomvi wa wachuuzi/machinga na polisi Kenya, au mumesahau huko kwenu haya ni mambo ya kawaida...


Acha kulinganisha Kenya na Tanzania, ukiangalia matukio yote ya Tanzania ni kwamba hawa wamachinga wamepewa sehemu maalumu za kufanya biashara, ila wao hawataki wanataka kufanya maeneo wanayopenda wao, jeshi la polisi linalokifanya ni kuwafukuza kwa kufuata sheria na taratibu za nchi, hakuna kuchukua wala kuiba mali zao kiholela kama huko kwenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi huyu MK254 ni mkenya kweli au ni furushi flani la kitanzania linalojivika ukenya! Em fuatilia kiswahili chake ni pure kabisa tofauti kabisa na wakenya walio wengi ila pia post zake nyingi hua anawaponda ccm which means yeye ni mfuasi wa upinzani.. Hivi kwa logic tu ya kawaida mimi kama mtanzania nawezaje kuwachukia odm au jubilee, chochote kati ya hivyo vyama kinaniathiri vp mimi kama Mtanzania hadi nikichukie au kukipenda? Hawa sio wale watz jamii ya hamorapa na mr nice ambao wakikaa Kenya siku 2 tu wanajiita wakenya? Mi hili gunia linalojiita MK254 siliamini kabisa litakuwa litanzania kabisa basi tu limeamua kujitoa akili
 
Kama Hupendi kujisifu you are a walking corpse
 

Umesababisha niangue kicheko sana hapa, mimi siichukii CCM, wala Tanzania, ila sipendezwi na tabia zenu MaCCM wa kwenye mitandao ya kijamii hususan mliojazana kwenye hili jukwaa la taarifa za Kenya, mumesheheni uzandiki uliokubuhu, maana yaani kile kile mnachoanika kama mapungufu ya Wakenya, unakuta huko kwenu mnakifanya mara kumi zaidi.
Mleta mada kakurupuka alfajiri kuleta taarifa za ugomvi wa polisi na machinga na kutumia kama kigezo cha kutusimanga sisi Wakenya, ila amesahau mikimbio na malumbano baina ya machinga na wana usalama huko kwenu ni jambo la kawaida sana.

Hata hivyo usitie hofu wala mashaka kuhusu utaifa wangu, mimi Mkenya tena mzalendo kupita maelezo, sema huwa napenda kutinga kwenye hiki kijiwe cha Ke vs Tz kupashana na Watz ili kujikumbushia soga za Wabongo, niliwahi kuishi kwenu huko na nikakatiza mikoa mingi zaidi ya wengi wenu.
Usiwe unapanic na mambo ya humu, mwisho wa siku haya mataifa hutegemeana, melfu ya wafanya biashara hunufaika sana kwenye uhusiano uliopo baina ya hizi nchi mbili.
Kwa taarifa yako kuna Watz wengi humu nimewahi kuwasaidia au kuwaelekeza kwenye masuala ya kibiashara Kenya kupitia inbox....nothing personal.
 
Haha! Unawachanganya wengi humu JF kwa Kiswahili chako sanifu. Mwanzoni nilidhani labda wewe ni mwalimu wa Kiswahili nchini Kenya. Big up, brother...
 
Duh MaCCM mumeishiwa kweli hadi mumekimbilia kwenye taarifa za ugomvi wa wachuuzi/machinga na polisi Kenya, au mumesahau huko kwenu haya ni mambo ya kawaida...


Hatuhitaji ufananisho , tunahitaji ujibu hoja za mleta mada.
 
😀😆haya bana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…