Hawa kweli ni wanangu?

Kaka unachokitafuta sio kizuri sana, halafu umeshakua na akili ya kuzijua dalili za mtoto uliebambikiwa sasa usichimbe zaidi ya hapo, ndoa ina changamoto sana hasa ukijua mkeo amekusaliti utakua na msongo wa mawazo.
 
Watoto ni wako. Nakupa siri kwenye hizo tare.

Hapo kwenye Tarehe Ongeza 7 na kwenye mwezi toa 3.

Mzee tarehe ni hizo hizo na Mimba za Mapacha zinawahi kuzaliwa kuliko ya mtoto mmoja.

Ungekuja na sababu ya kwamba Mwanamke ana wa aume wengi na hajatulia hapo sawa.
 
Msilete huruma kwenye maisha ya watu. Akawapatie baba yao halali na mimi nikalee ambao ni wangu halali. So far sijaacha kuwalea mpaka sasa
Kumbe na wewe umezalisha njee ya uchumba wako huu ukamkacha mwana na mama yake ukatafuta mchumba mwingine halafu uliokua nae kakuletea wana sio wako huoni hiyo ni karma kaka
 
NAKUSHAURI LEO HAO WATOTO MAPACHA BILA UBAGUZI, ikiwezekana mwambie mama yao kuwa unatambua siyo wako ila unalea kwasababu hao watoto hawana hatia. Pole na hongera
Alee watoto ambao si wake? We mjinga nini.

Unaweza kuhangaikia mkojo wa mwaname mwenzako? Basi kule siku hizi ni kwepesi sana au wenzetu pesa mnaziokota?
 
Maana ya hiyo kauli ni kwa mke wa ndani. Mimi huyo hakuwa mke wangu. Nlikutana nae tu kisela
Ndo hivyo uwe umekutana naye au la watoto wameshakua wako. Kwa ushauri zaidi kapime DNA
 
Kaka unachokitafuta sio kizuri sana, halafu umeshakua na akili ya kuzijua dalili za mtoto uliebambikiwa sasa usichimbe zaidi ya hapo, ndoa ina changamoto sana hasa ukijua mkeo amekusaliti utakua na msongo wa mawazo.
Huyu sio mke wangu mkuu. Nafikiri utakuwa haujasoma vizuri mkuu.
 
Mkuu sijasema
Kumbe na wewe umezalisha njee ya uchumba wako huu ukamkacha mwana na mama yake ukatafuta mchumba mwingine halafu uliokua nae kakuletea wana sio wako huoni hiyo ni karma kaka
sijakosea au sina makosa. Mada hapa ni kwamba kuwalea nshakubali wala silalamiki juu ya hilo. Issue hapa ni uhalali wa watoto kama ni wangu au lah!
 
Cha maana ni matunzo / kulea hayo mengine ni sperm donor; Utakuwa wa maana sana katika ustawi wa huyo mtoto kama mlezi kuliko absentee father (hata kama sio wako wewe ni wa maana zaidi kuliko huyo so called wake ambaye hayupo)

Ignorance a bliss... wewe swaga twende achana na uchunguzi ambao mwisho wa siku outcome zake huenda zikawa na hasara kwa wahusika...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…