Hawa masheikh wa Dar ni nani kawatuma?........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184


Amiri wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Mussa Kundecha (kushoto), akijadiliana jambo na Mjumbe wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Shehe Ally Bassaleh, wakati wa kutoa tamko la waumini wa dini hiyo, Dar es Salaam jana kuhusu mauaji ya watu watatu katika ghasia za kisiasa zilizotokea Arusha hivi karibuni. (Na Mpigapicha Wetu).
 
Masheikh wa Dar wanaendesha shughuli zao kidektate tu wala hawafanyi mawasiliano na wale wa mikoani kujua wanataka nini na huamua kuwaburuza tu....................................Huu ni udikteta.......................haiwezekani masheikh wachache kutoa tamko la kuwagusa waislamu wote nchini hata bila ya kuwasiliana nao............................
 
Hao mashekhe wametumwa kuimarisha neno udini kuwa lipo na ndio wanataka kumwonyesha JK kuwa hilo janga la udini lipo.yaani kuna viongozi wengine wa dini zetu kweli sijui ni njaa au? kwanini mtu asiangalie ubinadamu anatumia dini kutoa tafsiri tofauti katika jamii,
 
ushasema sheikh maana yake mdini tayar naona unapata tabu.masheikh wamewasiliana na sisi waislam nchi nzima hata arusha wajumbe walienda n.k. Waislam kama kundi jamii lazima watoe msimamo na utakua tofaut na ule wa maaskofu na vyama vya siasa
 
ndio maana mapadre mashoga nao walipigania haki zao nakanisa likawatambue
 
Walichosema masheikh ulikisiliza lakin au uliboreka kuona kanzu nakilemba?
 
Waislam wanasema wao ndo walimpokea nyerere dar na wakampa uenyekiti baadae aliwageuka nakukandamiza mpaka leo ndo maana tabora na moshi tofauti huku kumeendelezwa kwingine kumedumazwa
 
Sikusuudii kumshauri mtu hapa kwa kuwa najua aidha nishauri au nisishauri kutakuwa na mambo mawili:

  1. "Waislam" hawataelewa kwa sababu wao kikubwa kwao ni kuwa tofauti tu na "Wakristo" hata kama tofauti hiyo haina mantiki. Elimu.
  2. Kupinga kila kitu kwa kigezo cha "tunaonewa, tumenyimwa mahakama yetu, ......" hakutasaidia kwa kuwa hoja zinazoonekana ni za "Wagalatia" zitaendelea kupamba moto. Pressure ya katiba mpya ilianzishwa na "Washenzi sana hawa Wakristo" wa CHADEMA na kwa hakika moto huo hautazimika. Pili mahakama ya kadhi haitaweza kulipiwa na serikali hata kama wataandamana na kuua au kujiua. Tatu Mwenyezi Mungu ambaye ni wetu sote Waislam na wasio Waislam ataendelea kubariki na kulinda Watanzania wote wanaoipenda nchi yao na wale wanaotaka kugombana na Wakristo ilhali hawataki kuacha UZINZI na UVIVU WA KUFANYA KAZI NA KWENDA SHULE hawataingia peponi.
Nasikitikia Watanzania wenzangu kwa kuwa wana masikio lakini hawasikii, wana macho lakini hawaoni na hata wakiona hawatambui. Mapamabano yaendelee. Katiba yaja.
 
....waliohudhuria huo mkutano wa Karimjee, tamko gani lilitolewa juu ya ufisadi nchini, katiba mpya, ukosefu wa ajira, mikataba ya kitapeli ya kinyonyaji baina ya serikali ya CCM na 'wawekezaji', mmomonyoko wa maadili katika jamii, ukosefu wa uzalendo, kushuka kwa thamani ya shilingi, kupanda holela kwa gharama za maisha? kama hakukuwa na matamko kama haya, nawasihi kawaombeni tena JK na Makamba pesa za ku-facilitate gathering nyingine mjadili mambo kama haya!!!! anyway japo najua hamna shule ya kujadili ishu nzito kama hizi, jitahidini hivyo hivyo kimadrasa madrasa!!!
 
ndio maana mapadre mashoga nao walipigania haki zao nakanisa likawatambue

Tangu zamani nilijua uwezo wako wa kufikiri ni mdogo, lakini zikudhani ni mdogo kiasi hiki ulichokionesha hapa.
 
ushasema sheikh maana yake mdini tayar naona unapata tabu.masheikh wamewasiliana na sisi waislam nchi nzima hata arusha wajumbe walienda n.k. Waislam kama kundi jamii lazima watoe msimamo na utakua tofaut na ule wa maaskofu na vyama vya siasa

ndiyo, msimamo unaotolewa na mashehe lzm uwe tofauti na ule wa viongozi wa kikristo kwa kuwa wanatoka nchi tofauti au?. Shame upon you wewe unayesherehekea kwa kuwa aliyekufa si wa dini yako.
 
Kosipokuwa na maono jamii hupotea. Watu wajifunze kujadili hoja na si personalities, maaskofu wa Arusha wamelisemea suala la kutofuatwa kwa taratibu za uchaguzi wa Meya ambalo ni jukumu la kila mwananchi. Sasa wanapoibuka watu wengine kuitisha mkutano na kwa kulipia gharama ya ukumbi kwaajili ya kuwapinga kwa kuamini kuwa walichokifanya ni udini haiingii kwenye akili yangu. Kama ni udini ni udini dhidi ya dini ipi? Meya aliye chaguliwa pamoja na naibu wake ni wakristo namaaskofu waliotoa tamko kupinga ni wakristo, hivyo nilidhani kuwa hapo suala la udini halipo bali ni kupiga taratibu zilizotumika. Waliouwawa Arusha ni wakristo na waislam, hakuna udini hapo.

Jamii yetu iwe makini kutotumiwa na wajanja kuhalalisha mambo yao.
 
Uwezo wao wa kuchanganua mambo kwa kina ni mdogo sana ndiyo maana wanatoa kauli ambazo zinaonyesha wazi kwamba wanatumiwa na kundi la watu wachache ili wakidhi matakwa yao.
 
ushasema sheikh maana yake mdini tayar naona unapata tabu.masheikh wamewasiliana na sisi waislam nchi nzima hata arusha wajumbe walienda n.k. Waislam kama kundi jamii lazima watoe msimamo na utakua tofaut na ule wa maaskofu na vyama vya siasa


acha uwongo mbona mimi niko msikitini sijasikia hau mnawasiliana usiku wa manane?Nilazima kuwe na uwiano wa taarifa maana kutumika au kutumiwa si vema.madai ya masheikh siku zote yamekuwa ni mvurugano nakiri hata katika msikiti niliomo vurugu hizi haziishi lakini si waislam wote tunayapenda haya.
 
Are you for real!?
 

Mimi swali langu kwao ni hili: Kama udini upo Tanzania, ni kwa nini wanaona udini kwa wengine tu (maaskofu) na siyo kwao pia?
 
Hivi kumbe mnakaliaga vitu uhuu nilidhani ni MIKEKA TUU:smile-big:
 

Kaka huu ubinadamu kwa nini uelemee upande mmoja? wakati waandamanaji wa CUF zaidi ya 100 walipouawa na Polis Zanzibar sababu ya haya haya maandamano, mbona hatujasikia kauli ya Maaskofu wakilaaani, au hawa walikuwa Mbuzi? matokeo yake Maaskofu walipongeza Geshi la Polis kwa kulinda na kuidumisha amani ya inji. kwao wao Maaskofu kuuliwa watu kule Zanzibar ilikuwa ni kudumisha amani ya inji, lakini kuuliwa wafuasi watatu wa Chama wanachokisapoti wao Maaskofu cha CHADEMA imekuwa headiline makanisani, kama huu si udini ni nini? tukubali tukatae CHADEMA ni chama cha kidini na misingi yake ni ya KIKRISTO na ndo maana Mgombea wake Padri Slaa alikuwa na baraka za Kanisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…