Hawa Mchafu aongoza mafunzo ya biashara kidigitali kupitia LHRC

Hawa Mchafu aongoza mafunzo ya biashara kidigitali kupitia LHRC

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani (UTW) Mhe. Hawa Mchafu ameambatana na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Right Center - LHRC) Wakili Anna Henga; Mbunge Jimbo la Bagamoyo Mhe. Muharami Mkenge; Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo Mhe. Mohamed Usinga na viongozi wengine kwa pamoja wametembelea mabanda ya biashara na kuona kazi za wajasiriamali wanawake Wilayani Bagamoyo.

Wanawake wajasiriamali Wilaya ya Bagamoyo wamempongeza Mhe. Hawa Mchafu kwa kuleta mafunzo ya biashara kidigitali kupitia LHRC ambapo lengo la mafunzo hayo ni kukuza biashara zao kiteknolojia.

"Teknolojia inasaidia sana kukuza biashara nyingi kupitia mitandao mbalimbali, tuendelee kuitumia kibiashara zaidi" - Mhe. Hawa Mchafu, Mbunge Viti Maalum CCM - Pwani

Mhe. Mchafu amesema; "Asante sana sana Wadau wetu wa Maendeleo, LHRC kwa Ibada hiii ya Mafunzo kwa Wanawake wajasilimali zaidi ya 300 Katika Wilaya yetu ya Bagamoyo Mkoani Pwani juu ya Masuala ya Biashara Mtandao, Ubunifu sambamba na Technologia, Ukatili wa Kijinsia na Msaada wa Sheria."

"Shukurani zangu za kipekee zimuendee Mkurugenzi Mtendaji Wakili Msomi Dada yangu Madame Anna, Hakika mmefanya jambo kubwa sana sana jambo la Kimungu jambo la Ibada kwani Wanawake hawa wakifanikiwa katika biashara zao kwa kuongeza ubunifu na elimu mliyowapatia ama hakika watazikomboa Familia zao na watajikombea kiuchumi pia." - Mhe. Hawa Mchafu

"Tunawashukuru sana kwa kuamua kuunga Mkono kwa Vitendo juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za Kutoa Mabillioni kwa Wanawake Wajasiriamali na wafanya biashara wadogo kupitia 10% yaani ( 4,4,2) na kuifanya iwe kwa Mujibu wa Sheria na inatolewa bila ya Riba" - Mhe. Hawa Mchafu

"HAKUNA KITAKACHOSIMAMA NDANI YA MKOA WA PWANI".


WhatsApp Image 2023-03-04 at 22.06.26.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-04 at 22.06.25.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-04 at 22.06.27.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-04 at 22.06.28.jpeg
 
Back
Top Bottom