Wana JF
kwanza, lazima tukubali kuwa kila mtu anamtazamo wake katika kuchambua au kuangalia suala fulani na ni haki yake,
Pili, kila mtu ana haki yake ya kidemokrasia kushabikia upande fulani na hakuna mtu mwenye haki ya kutaka kujua kwanini ni shabiki
Tatu, kina mtu yuko huru kuwa mwanachama wa chama chochote hivyo akajisikia anawajibu wa kusemaa chama chake 'positively'
Nne, Kuna baadhi ya watu hawako katika kundi lolote kazi yao ni kuwa critical katika masuala mbalimbali bila kujari ni la chama gani
Tano, JF ni jukwaa huru kwa mtu yeyote bila kujari yuko upande gani katika makundi niliyotaja hapo juu
Kwa mantiki hiyo si sahihi kwa wale ambao wanakuwa na mawazo tofauti hasa na wale washabiki na wanachama na wapenzi wa CHADEMA kuanza kusakamwa, kuonekana hawafai, kuwatukana n.k
Wale wanaJF ambao wamekuwa wanawasakama wanaJF wngine ambao wametofautina nao kimawazo, kiitikadi na mitazamo ni namna ya kuonyesha ufinyu wa mawazo, kutokomaa kimawazo na udikteta wa mawazo. Wanatakiwa kubadilika kimawazo wawe wanajibu hoja kwa hoja badala ya kutukana na kukashfu wana JF wengine.
Wana JF hao wakumbuke kelele za chura hazimzii ng'ombe kuywa maji, la msingi ni kufanya uchambuzi wa kina wa hoja na kuona wapi palekebishwe kwa manufaa ya baadae, hivyo kwa namna fulani wan JF tuwe kama pressure / lobbying group kwenye society ili kurekebisha mambo.
Kama mtindo utakuwa wa namna hii JF itakuwa kama jukwaa la MBAYUWAYU ambapo nafikiri hata founders wetu wa JF wasingependa tuwe mbayuwayu ila wangependa tufanye kitu cha kuleta mabadiliko katika jamii yetu