Hawa ndio aina ya wanawake anaovutiwa nao msanii A.K.A kutoka South Africa!!

Hawa ndio aina ya wanawake anaovutiwa nao msanii A.K.A kutoka South Africa!!

Edger ngassa

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2015
Posts
294
Reaction score
239
A.K.A (A.K.A Worldwide) ni msanii maarufu kutoka
Cape Town South Africa ambae miezi michache
iliopita alialikwa jijini Dar es salaam kuperform
kwenye party ilioshika headlines kubwa; Zari All
White Party . Msanii huyu anafahamika kwa hit
songs zake kama Congratulate na All Eyes on Me
aliomshirikisha msanii Burna Boy kutoka Nigeria.
Nimekutana na interview moja aliofanya msanii
huyu nchini Nigeria na moja kati ya maswali
alioulizwa A.K.A ni kuhusiana na aina ya
wanawake anaovutiwa nao. Najua watu wengi
watasema labda wanavutiwa na sura au umbo la
mwanamke lakini mtazamo wa A.K.A ni tofauti
kidogo, yeye alikua na haya ya kusema:
A.K.A >>> “Wanawake wanaonivutia mimi sio
wenye sura nzuri sana wala umbo zuri sana bali
wenye upeo wa kuona mbali, mtu ambae haishi ili
mradi tuu bali anaishi kwa malengo, pia mimi
zivutiwi na wanawake ambao hawanipi msukumo
wowote ule maishani mwangu, navutiwa na
mwanamke ambae ana msukumo wa kufanya vitu
vikubwa kwa sababu kwa dunia tunayoishi sasa
kama huna ndoto za mbali usitegemee utakua na
mwanamke ambae ana mawazo hayo pia, ukweli
huo pia upo kwa wanawake vile vile” .
Swali lingine aliloulizwa lilikua kama angepewa
nafasi ya mwisho kuperform nyimbo yoyote ya
kwake duniani, angechagua kuperform nyimbo gani
na kwanini?
A.K.A >>> “Duuh! kama ningepewa nafasi ya
kuperform mara ya mwisho duniani basi
ningeperform nyimbo yangu ya Congratulate
kwasababu ni nyimbo nilioiandika wakati ambao
nilikaa na kutazama nilipotoka na kuona kua
nimepiga hatua nzuri kimuziki kwani muziki wangu
ulikua umeanza kutoka na kupigwa katika nchi
mbali mbali za Affrica, kwangu kitu hicho kilikua na
hatua ya mafanikio, so nikaamua kutoa nyimbo
kujipongeza.
 
Back
Top Bottom