Hawa ndio Ccm ni wale wale Jana Leo kesho na hata milele

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Ukiusikiliza ule wimbo wa Ccm mbele Kwa mbele Kuna maneno yanimbwa " Ccm ni Ile ile na makali ni yaleyale" hii nikweli

Vijana kama mnategemea sisiyemu itawalete kitu kipya sahauni sana sana wanaboresha namna ya kuifisadia hii Nchi.

Kikwete si alituahidi ajira Kwa Kila kijana?
Magufuli si alisema vilevile?

Subiri na huyu mama atasema yaleyale mko hapa.

Kikwete alienda mbali zaidi Kwa kusema "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA."

Katika uongozi wake nadhani mwaka 2006-2007 kulikuwa na njaa Kali mno tulikula mtama kama hatuna wazazi hii ilipelekea Hadi tukawa tunapewa mahindi Bure ya msaada.

Ng'ombe walikuwa hawana bei ilifikia ng'ombe tunauza Hadi 20,000/= ndio ni elfu ishirini Wakati kwenye kampeni alituambia maisha Bora Kwa Kila MTANZANIA!!


Hawa ndio ccm
 
Ajira zimeanza kuwa janga miaka ya mwisho ya urais wa mkapa until then hakuna mtu atakaye kuja kubadirisha hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…