Hawa ndio mastar wa 5 wa bongo ambao wametoka familia za kishua

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304



Hakuna mtu asiyejua maana ya watoto wa kishua basi kama yupo basi maana halisi ya neno hili ni wale watoto waliozaliwa kwenye familia zinazojiweza au unaweza kuita familia Bora. Mara nyingi wasanii wengi huwa wanatokea maisha duni na kupigana na maisha hadi kufikia walipo sasa. Kipindi Diamond akiacha shule kwa kukosa pesa ya kumsomesha nana elimu yake kuishia A'level , Hawa wengine walikua wapo shule wakisoma na kuishi vizuri. Vibe Tanzania inawaorodhesha baadhi ya watoto wakishua ambao kwasasa ni celebrities…


Vanessa Mdee

Vanessa Hau Mdee au unaweza kumuita Vee au Vee Money alizaliwa mjini Arusha mwaka 1988. Vanessa mdee alikuzwa na baba yake Sammy Mdee (kwasasa ni marehemu )ambaye alikua ni mtu mzito kwenye nchi hii na mama yake sophia. Akiwa na umri mdogo Vanessa aliweza kusafiri nchi mbalimbali duniani. Vanessa Mdee alikulia miji ya New York , Paris , Nairobi na Arusha.


Nisher
Nisher ni mtoto wa Mtumishi wa Mungu Mh Nabii GeorDavie anayeongoza huduma ya Ngurumo ya Upako yenye makao yake jijini Arusha. Nisher amekulia katika maisha mazuri na hadi ni wakishua bado. Baba yake aliweza kumsaidia Nisher kufungua studio yenye thamani kama ya milioni 15 ili mtoto wake aendeleze kipaji alichonacho.




Jokate Mwengelo
Huyu unaweza kumuita mtoto wa Oysterbay kwani ndio alipokulia huku baba yake akifanya kazi serikalini. Kumbuka Jokate alizaliwa washington DC nchini Marekani ambapo wazazi wake walikua wakifanya kazi huko. Alipomaliza high school katika shule ya Loyola ndipo alipogombania Miss Tanzania mwaka 2006 na kushika nafasi ya 2.



Lucci

Jina lake halisi anaitwa Luciano Tsere au unaweza kumuita Lucci ambaye ni producer maarufu nchini. lucci amezaliwa tarehe 30 September mwaka 1985 Lusaka Zambia, akiwa ni mzaliwa wa nne, wa mwisho kuzaliwa na akiwa mtoto wa kiume pekee kwenye familia yao. Lucci naye kama jokate amekulia Obey kwenye familia bora ambapo kwasasa mzee wake ni balozi wa Tanzania.



Wema Sepetu
Wema Sepetu ni msichana anayetoka kwenye Familia ya kibalozi akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia ya wasichana wanne wa Balozi Isaack Sepetu Ibrahimu (marehemu).Wema sepetu alizaliwa mnamo mwaka 1988 katika hospitali ya ST. Andrew's jijini Dar es Salaam na ni mtoto wa mwisho kuzaliwa huku akisoma elimu yake ya primary na sekondari katika shule ya ACADEMIC INTERNATIONAL iliyopo jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Nchini Malaysia kusomea mambo ya biashara za kimataifa katka chuo cha Limkokwing University.

Wema mshaona sana picha zake ndio maana hapa sijaiweka


 
Diamond na jaydee sawa hao wengine hawajatoboa bado
 
Huyo lucci kakulia arusha hiyo obey ameijua akiwa na miaka 20 mana walihamia dar 2006 baba yke alipoteuliwa kua dc,huyo nisha nae walewale 2007 baba yake alikua na ki celica kibovu ndio dogo alikua anaendesha mitaa y kisongo maisha yao yameanza badilika 2010 so sio wa kishua huyo
 
Tuletee na list ya masikini wa 5 ambao wametoboa

Mkuu
Upo sahihi nadhani mtoto ambaye ameibuka toka familia maskini anahitaji pongezi zaidi kwani tunajua hawa watoto wengine wanavyobebwa na majina makubwa ya familia wanazotoka.
 

kwani kukulia Arusha ndio umasikini,nenda Arusha kajionee
 
kwani kukulia Arusha ndio umasikini,nenda Arusha kajionee


Acha ubishi Wa kijinga kubali umechapia we si ndo umeleta habari kuwa kakulia obey Ili kumnasibu ni WAKISHUA?

Teh teh muwe mnaedit info zenu kabla ya kukimbilia kuanzisha thread....
 
hata laki si pesa nae ni mtoto wa kishua baba alikua balozi marekani ila amesha staafu yupo kijijini namtumbo.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…