mr gentleman
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 3,222
- 4,689
Kwa mujibu wa utafiti wetu wa miezi miwili tumegundua awa ndio vijana wenye nguvu na wanaokubalika zaidi hapa Tanzania kwa sasa. Utafiti huu umeshirikisha members wenzetu mbalimbali.
Tulizingatia haya yafuatayo
Nguvu yake kwenye mitandao ya kijamii
Anavyopokelewa kwenye mikusanyiko
Kutajwa kwenye vyombo vya habari
Na mchango kwenye jamii yake
Vijana awa ni wafuatao
1. Diamond platnumz
Aka Dangote au Sukari ya Warembo, uyu ni kwa sasa ndio msanii namba moja wa bongofleva. Ana ushawishi mkubwa sana kwenye industry ya muziki afrika ya mashariki na kati, show anazofanya zinavuta watu wengi haswa vijana. Diamond ni balozi wa coca cola, mziiki, dstv. Ndio msanii anaelipwa pesa nyingi kwa sasa afrika mashariki na kufanya matamasha kwa bei mbaya sana. Kwa sasa Diamond ndie biashara kubwa kwenye tasnia ya sanaa Tanzania na East Africa.Kinachomfanya D kuwa msanii wa kipekee sio miujiza bali ni ubunifu, kufanya kazi kwa bidii, kuwekeza kwenye kazi yake na good marketing strategies.
2. Zitto kabwe
Mwanasiasa kijana anaekubalika na watu wa kada zote, itikadi zote na rika zote. Ndio amewashawishi vijana wengi kuingia kwenye siasa kutokana na misimamo yake, mitazamo yake na ushawishi wake kwenye kujenga hoja. Kwa sasa hana maelewano mazuri na chama chake cha chadema ila nguvu yake bado haijatetereka na ushawishi wake kwa vijana ni mkubwa mno. Zitto anakubalika kutokana na kuweka wazi mitazamo yake na kuisimamia.
3. Lady jaydee
Maarufu kama ‘Komando' au ‘Anaconda' majina yake tu yanaweza kukutambulisha uyu ni mwanamama wa aina gani. Ndio msanii anayeongoza kwa kuwa na mashabiki wengi afrika ya mashariki, ni CEO wa Nyumbani lounge, anamiliki Machozi band, ni balozi wa oriflamme, marie stopes na ana biashara zingine nyingi. Uyu dada ni hustler na hapo alipo ana tuzo nyingi mpaka pakuziweka pamekosekana.
4. Patrick Ngowi
A.k.a billionea mtoto ni kijana mchakarikaji anayedhiirisha kwamba hard work pays alianza na biashara ya simu na kuamia kwenye solar, anatengeneza pesa chafu sana kutokana na biashara yake hiyo ni tishio la baadae kwa kina Mengi, Bakhresa na Rostam. Anatambulika na Forbes na tahasisi nyingi za kimataifa kama mfano mzuri kwa vijana wa kiafrica.
5. Ruge Mutahaba
Uyu ni master mind wa tasnia ya burudani Tanzania, ndio roho ya clouds media kwa sasa. Kijana uyu wa kihaya ana ushawishi mkubwa sana kwenye muziki na biashara ya sanaa kiasi kwamba kuna wanaoamini ndio upanga kila kitu na wengine kufata alichopanga, ushawishi wake upo mpaka Ikulu. Nafasi yake pale Clouds media haieleweki vizuri maana amekaba kila angle almaarufu "kiraka". Ndio mmiliki wa tahasisi ya vipaji ya watoto yatima (THT), mmiliki wa Pera Africa kampuni ya ringtones na callerback tunes, pia Ruge ni mmiliki wa mtandao mmoja mpya wa kuuza kazi za wasanii na biashara zingine ikiwemo kusimamia wasanii na kuandaa matamasha ya muziki mfano tamasha la injili.
6.Flaviana Matata
Mwanamitindo anayeeshimika na kuiwakilisha vizuri sana Tanzania kimataifa katika anga za mitindo na kugeuka kipenzi cha vijana wengi haswa wa kike. Flavi kwa sasa anafanya shughuli zake nchini Marekani na amefanikiwa kufanya kazi zake na makampuni makubwa ya mitindo duniani.
Nje ya kazi yake ya fashion Flavi pia ni mshiriki mzuri wa shuguli za kijamii kupitia tahasisi yake, amekuwa akichangia elimu maafa na vinginevyo.
Huu ndio utafiti wetu na matokeo yake, lengo lilikuwa kupata vijana kumi ‘wa nguvu' lakini tunasikitika tumeangaika sana lakini tumeishia vijana awa sita tu. Ila kama kuna unayetaka kumwongezea unakaribishwa.