Hawa ndio washindi wa tuzo za watu

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
Mtangazaji maarufu Salim Kikeke wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC ametwaa taji la Mtangazaji wa Runinga Anayependwa katika toleo la kwanza la Tuzo za Watu za Tanzania au Tanzania People’s Choice Awards katika sherehe zilizofanyika Serena Hote, Ijumaa jijini Dar Es Salaam.
Vipengele 11 (kumi na kimoja) vilikuwa vikishindaniwa. Mshindi katika kila kipengele ameibuka na zawadi ya shilingi milioni moja pamoja na tuzo. Chini ya orodha ni picha za tukio hilo.

ORODHA YA WASHINDI
1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA
Millard Ayo – Clouds FM
2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA
Amplifaya – Clouds FM
3.MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA
Salim Kikeke – BBC Swahili
4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA
Mkasi – EATV
5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA
Juma Kaseja – Yanga
6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA
Nisher
7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME
My Number One – Diamond
8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE
Yahaya – Lady Jaydee
09. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
King Majuto
10. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
Elizabeth ‘Lulu’ Michael
11. FILAMU INAYOPENDWA
Mkongwe King Majuto akiwapa mashabiki wake heko kwa kumpigia kura. Ameshinda kipengele cha Muigizaji wa Kiume Anayependwa Kwenye Filamu. Pembeni ni Lulu Michael, mshindi wa Mwigizaji wa Kike Kwenye Filamu Anayependwa.
Picha ya pamoja ya walionufaika katika Tuzo za Watu mjini Dar Es Salaam, Juni 27, 2014.
Salim Kikeke wa BBC Dira ya Dunia, mshindi wa kipengele cha Mtangazaji wa Runinga Anayependwa, akizungumza machache baada ya kutangazwa.
Ndoa Yangu
 
HONGERA zao wote waliopata tuzo hizo..!! Nimepanda sana vipengele ktk kuwania
tuzo hizo na zaidi nimeona jinsi gani tuzo hizo zinavyokuja kwa kasi na kupendwa zaidi!! BIG UP SANA TUZO ZA WATU!
 
Lulu anapendwa mnoo etiiii !!!!"!!hafi maskini lulu maana najua atautumia uchumi wake vizurii sijui salim kikeke kaponaa hapoo
 
Hell no,yule ni kama baba yangu bwana angekua kijana walau wa 30's kidooogo sawa

Uzee namba tu hata kene kalkyuleta zipo,we jamaa anauzee gani huyo,kikwete mwenyewe anajiita kijana
 
Mh kote nimekubali..ila hapo pa lulu ni shada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…