Hawa ndio watakaookoka na kumuona Yesu Kristo

Hawa ndio watakaookoka na kumuona Yesu Kristo

MIRA01

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2023
Posts
319
Reaction score
695
Naomba niweke hili wazi kabla sijaendelea na hiii mada kwenye kurasa huu, sipo hapa kuhukumu wala kukosoa imani ya mtu yeyote yule kuanzia kwenye madhehebu na iman na dini tofauti

Moja ya vitu ambavyo wakristo wengi wanapambana navyo kwenye kipindi hiki cha mwisho wa kufunga historia ya ulimwengu huu ni hii ni kuwavuta na kuwashawishi watu wengi waamie kwenye madhehebu yao ama iman zao,

Kiukweli ni wakristo wananiru juu ya ujio wa Yesu kristo mara ya pili ulimwenguni, hilo sizan kama kuna mtu ama dini anabisha kuhusu hili kwa maana lipo wazi kwenye vitabu vyote vya iman. Sasa niwatoe hofu watu wote ambao kazi yao nikuwaaminisha madhehebu yao ndio njia na ya kweli ya watu kwenda mbinguni!

Ni wazi ya kwamba wanakosea sana na ni wazi ya kwamba wanawadanganya watu wengi na wengi hupotea kwa sababu hizo maana wanaingia makanisan ambapo huenda kuwaamin watumishi wao ambao wengi ni wauongo na mara hufadhaika miyoyoni mwao na kuona na kukana imani zao.

Mungu wa mbinguni anawatu wake maeno yote ya ulimwengu, nao ni WAKRISTO na sio wa dhehebu fulani l, watu hao wapo maeneo yote ya ulimwengu huu, wapo makanisani kwa waroman wapo kwa walutheli wapo pia kwa walokole na makanisa ya kikristo ulimwenguni kote, Mungu huwajua watu wake na watu wake wanamjua na kumuamini wanayemuabudu na sio kuwa na iman yao kwenye makanisa ama madhehebu ya makanisa ya Kikristo.

Sasa nawashangaa zaidi watu wanaowalazimisha watu wengine kushiriki kwenye makanisa yao ambayo mengi kwayo ni milango ya kuingilia kuzimu kwa sababu kila msingi wa kanisa na waanzilishi wao wana mission na vision zao na wanazitekeleza kila kitu.

Sasa kwann uangaike na kutangatanga kwwnye mambo mbayo hayatokupeleka popote hata mbinguni?

Muubirini kwa watu kwamba Yesu anawapenda muwafanye kuwa wanafunzi wa Yesu na sio wanafunzi wa kanisa fulani, na wakiamini basi msisite kuwa batiza kwa maji mengi na kuwakabidhi kwa YESU kristo ili wabatizwe kwa roho, ndilo agizo kuu la Bwana kwa mitume na watumishi wake.
 
Wapi Yesu anasema "mimi "Mungu"?
 
Halafu si mnasema Yesu tayari kishabeba dhambi za watu wote? Au kabaguwa watu?
 
Wakati wanamtafuta kristo. Na wenye makanisa wanaongeza bidii kuwanasa ndege wao kwenye biashara zao.
Hii ndio sababu imefanya niwaandikie uzi huu, biashara ya makanisa inawazamisha wengi motoni bila kuelewa nini wanafanya! Nimetoa mwanga watu wawe na aman na Mungu wao hakuna siku maalumu ya kumuabudu Mungu, yupo masaa 24 mtumaini yy peke yake na sio kanisa lako ama dhehebu lako
 
Chanzo cha madhehebu ni upotofu ,ukiona mtu anashabikia dhehebu na sio imani basi amepotea.
 
Yohana 14: 6-30

Hapa Yesu mwenyewe anajizihirisha kwamba Yeye ndiye Mungu
Yohana 14: 6 inasema
Yesu akawaambia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu.

Hapo Yesu anasema wazi kabisa kuwa YEYE NI MTUME aliyekuja na Njia sahihi na hakuna atakafika ktk ufalme wa BABA(MUNGU) Bila kupitia mafunzo yake.

Na hii ndio KAULI YA MITUME WOTE WA MUNGU.

Hakuna sehemu yyt Yesu kajiita MUNGU.

Wacha kabisa kusema uongo mbele ya wasomi.
Biblia tunaifahamu kuliko nyie mnaosema Uongo juu ya Mtume wa MUNGU Yesu mwana wa Maria.

ANDIKO LINASEMA
Mungu sio mwanadamu wala si mwana wa binadamu’ (Hesabu 23:19)

ANDIKO LINASEMA YESU NI MWANAADAMU.
Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja’ (Mathayo 16:27)

kwa sababu yeye ni mwana wa Adamu’ (Yohana 5:27)

ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu’ (Mathayo 12:40)

Vipi MUNGU aseme Yeye kamwe hana sifa ya kuwa MWANAADAMU Kisha ageuke ajiite mwanadamu?

Mnadai Mungu alikuja kwa umbo la binaadamu (Yesu) ili aishi kisha Afe km mtu.

Mnamkashifu Mungu hali mkidhani mnamsifu.

Biblia.

Biblia inasema kwamba Yesu alikana yeye ni Mungu
Yesu alizungumza na mtu aliyemuita ‘mwema,’ na kumuuliza, ‘Kwa nini unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu pekee yake.’ (Luka 18:19)

Biblia inasema kwamba Mungu ni mkuu kuliko Yesu
‘Baba yangu ni mkuu kuliko mimi’ (Yohana 14:28)

‘Baba yangu ni mkuu kuliko wote.’ (Yohana 10:29)

Yesu hawezi kuwa Mungu ikiwa Mungu ni mkuu kuliko yeye. Imani ya Kikristo kwamba Baba na mwana wako sawa ni kinyume kabisa na maneno yaliyo wazi kutoka kwa Yesu.

Kamwe Yesu hakuwaagiza wanafunzi wake wamuabudu
‘Mnaposali, semeni Baba Yetu uliye mbinguni.’ (Luka 11:2)

‘Siku hiyo hamtaniomba lolote. Mkiomba lolote kwa jina la Baba.’ (Yohana 16:23)

YESU NI MTUME wa MUNGU na kamwe SIO MUNGU
 
Halafu si mnasema Yesu tayari kishabeba dhambi za watu wote? Au kabaguwa watu?
Bibie mambo ,Yesu ameruhusu kusamehewa dhambi na kuwa mpya nasio anaendelea kubeba dhambi hapana alipunguza adhabu kali ya Mungu kwakubeba dhambi zetu past tense sio present nakufa kwake tumeokolewa ila kama unadhambi za sasa usipotubu utaenda motoni.

Ila kunadhambi ni ngumu kusamehewa kirahis .
1. Kuua
2 . Na kumtukana roho mtakatifu.
SAsa hizi dhambi husamehewi mf. Hii ya roho mtakatifu .

Ukiwa serious nitakuja kukufafanulia hadi ulewe. Na dhambi hizi kila ukienda kanisani kila ijumapili mnasemehewa dhambi zenu ila sio hizo nilizozitaja juu.

Dhambi ni kukosea amri kumi za Mungu .
Ukitaka kusamehewa dhambi zako ni unaanza nakufanya toba na kuwa msafi na kurudi kwa Mungu atakusamehea
 
Back
Top Bottom