Kama kweli Wabunge wetu ndio tumewachagua, ama kuteuliwa na Rais kutunga Sheria, halafu wao ndio wavunja sheria tuna kazi. Wanapigania kuondoa ufisadi, kumbe nao wanadhulumu wafanyakazi wao. Soma habari chini.
Zitto amkoromea Cheyo
Amtuhumu kunyanyasa madereva
na Charles Mullinda, Dodoma
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), juzi aligeuka mbogo wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Bunge na kumshambulia kwa maneno Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (DP), akimtuhumu kuwa ni mmoja wa wabunge wanaowanyanyasa madereva wao.
Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata kutoka ndani ya kikao hicho, zilieleza kuwa Zitto aligeuka mbogo baada ya kuibuka kwa mjadala wa madereva kudai mishahara na posho zao kutoka kwa wabunge.
Zitto alichukizwa na taarifa kuwa Cheyo ni mmoja wa wabunge sita waliowafukuza kazi madereva wao waliokuwa wakidai stahili zao ambazo zinatolewa na Ofisi ya Bunge kupitia katika akaunti za wabunge, lakini wamekuwa wakilipwa kiasi kisichojulikana.
Habari za ndani zaidi zilizolifikia gazeti hili, zilieleza kuwa Zitto alitofautiana pia na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo waliokuwa wakipinga hoja ya kutaka wabunge wote wawalipe madereva wao malimbikizo ya mishahara na posho nyingine zinazotolewa moja kwa moja na Bunge.
Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo waliokubaliana na Zitto ni Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama na Mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi, wote CCM, walisisitiza kuwa wabunge wote wanapaswa kulipa malimbikizo wanayodaiwa na madereva wao ili kuepuka kuingia katika kashfa ya kudhulumu.
Wajumbe wengine wawili, Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA) na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid (CUF), ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya upinzani, walibaki kimya bila kuunga mkono upande wowote.
Habari zilidai kuwa Zitto alimshutumu Cheyo kwa kumfukuza dereva wake kwa kosa la kudai malimbikizo ya mishahara na posho zake, jambo ambalo halikumfurahisha Cheyo, ambaye aliamua kujibu mapigo kwa kumtaka Zitto kutoingilia mambo yasiyomhusu.
Chanzo hicho kinaeleza kuwa baada ya Zitto kuona hoja yake ya kutaka wabunge walipe madeni wanayodaiwa na madereva ili kuepuka aibu ya aina yoyote inayoweza kuwapata inaelekea kugonga mwamba, aligeuka mbogo na kuwatishia wajumbe wenzake kuwa iwapo hawatakubaliana naye, basi atakwenda kuliweka wazi ili kila Mtanzania ajue madereva wanadhulumiwa haki zao na wabunge.
Tishio hilo la Zitto liliwafanya wajumbe wote kunyamaza, jambo lililobainishwa kuwa ni dalili za wabunge kukubali kwa shingo upande kuanza kulipa malimbikizo hayo.
Alipoulizwa kupitia simu yake ya kiganjani jana asubuhi, Cheyo alihoji sehemu ambayo gazeti hili lilipata habari hizo, kwa kuwa mambo yaliyotokea ndani ya kikao hicho yalikuwa siri.
Kwa ukali, Cheyo alisema hana ugomvi na Zitto, aliongeza kuwa kutofautiana kimsimamo au kauli ni jambo la kawaida ambalo linaweza kutokea kwa mtu yeyote.
Hata hivyo alishindwa kukanusha au kukubali madai ya kulumbana na Zitto katika Kamati ya Uongozi ya Bunge na kumfukuza dereva wake kwa kudai malimbikizo ya mshahara na posho zake. Alisema kwa mkato Zitto ni rafiki yake na anaheshimiana naye kwa kiasi kikubwa, kisha akakata simu.
Gazeti hili lilipowasiliana na Zitto katika viwanja vya Bunge jana asubuhi na kumhoji kuhusu kutokea kwa hali hiyo, alisema hawezi kuzungumzia mambo yaliyojadiliwa ndani ya Kamati ya Uongozi ya Bunge.
Wabunge wamekuwa katika mgogoro wa muda mrefu na madereva wao ambao wanadai kudhulumiwa mishahara na posho zao zinazopitia kwenye akaunti za wabunge.
Ofisi ya Bunge ilikwishatoa maelezo kwa wabunge kuwalipa madereva wao mshahara wa sh 100,000 kwa mwezi na posho ya sh 30,000 kwa siku wanapokuwa vijijini, katika majimbo ya uchaguzi wa wabunge, ambapo kwa mwezi wanapaswa kulipwa sh 300,000.
Habari zinaeleza kuwa maelezo ya Ofisi ya Bunge kwa wabunge, yanawataka kuanza kutoa mshahara na posho kwa kiwango hicho kwa madereva wao tangu Julai mwaka jana, hata hivyo, baadhi ya madereva wamekuwa wakiwatuhumu wabunge kwa kukaidi agizo hilo na kuwadhulumu stahili zao kama zilivyoanishwa na Ofisi ya Bunge.