MUWHWELA
Senior Member
- Oct 26, 2013
- 167
- 238
Habari wana jopo!
Ni furaha yangu kuwapo tena ndani ya jamvi hili la wafikirio chanya kwa mda mrefu kuliko wafikirio hasi..baada ya kupitia majarida,na maandiko tofauti katika vyombo tofauti vya habari,nimepatwa kidogo na mshituko juu ya wasomi hawa na waandishi hawa kujikita kushambulia watu kuliko kutoa hoja juu ya MCHAKATO WA KATIBA MPYA.
Hakuna asiyejua kwamba muungano wetu unamatatizo na kama hujui basi umeamua kutokujua kwa masirahi yako binafsi,lakini kwa habari ya kero za muungano zipo wazi,
Hoja yangu,rais wa zanzibar na rais wa jamuhuri,pamoja na wandamizi wao wakuu wa serikali hizi,ndio wanapaswa kuulizwa juu ya serikali tatu na si mh warioba,ikumbukwe kwamba rais wetu ndiye aliyeshindwa kuzuia mabadiliko ya katiba ya zanzibar ambayo katiba hiyo ilivunja rasim muungano wetu.
Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu,si muumini wa selikali 3 wala 2,mimi naamini katika selikali 1,ambayo rais wangu aliyopo madarakani ameshindwa hata kudhubutu kuelekeza watanzania kuelekea katika selikali moja,mtu yoyote ambaye ukweli kwake ni kitu cha thamani sana,ajiulize tangu kero za muungano zianze kwa nini viongozi hawa hawataki kutuuliza wananchi maswali mawili muhimu.
1-JE TUNATAKA MUUNGANO?
2-TUNATAKA MUUNGANO WA NAMNA IPI?
Rais wangu,waziri mkuu wangu,usalama wa taifa langu nilipendalo la tanzania, mtalaumiwa sana na vizazi vijavyo kwa hili,maridhiano yoyote ya kisiasa popote duniani msingi wake mkubwa huwa ni HAKI NA USAWA, baada ya vitu hivyo kupatikana mazungumzo yoyote hufanyika kwa ufanisi mkubwa.mmeshindwa kufanya maamuzi sahihi,kwa muda sahihi,itawagharimu duniani hata mbinguni,....
Watanzania wa leo si wale wa 77 ni watanzania ambao wanataka kuona neema katika taifa lao na siyo kuona machafuko,ila kama hekima yako ndugu rais na washika nchi wenzako itayumba,basi selikali iliyopo madarakani itapata shida sana mwishoni mwa kuondoka kwako na baada ya kuondoka kwako madarakani...BUSARA YAKO NA HEKIMA YAKO ITALIVUSHA TAIFA HILI SALAMA ----NAKUOMBEA KWA MUNGU,,,,
wanaharakati; najua machungu na jinsi ambavyo kazi hii ilivyo ngumu kuweni na msimamo usioyumba na acheni kuwa na matamko ambayo mnajua kuyasimamia matamko hayo hamwezi......WALIOWEZA WALISIMAMIA KILE WALICHOKISEMA
Mungu ibariki tanzania,mungu ibariki afrika