Hawa ndiyo wachezaji vitasa wa Simba SC wanaostahili kupongezwa na kupigiwa makofi watakaposhuka uwanja wa ndege


Hakuna anayestahili kupongezwa, malengo yetu hayakuwa kwenda kupambana, bali kwenda kuleta ushindi.
 
Huyo alikua anafanya makosa mengi na yalikua yanasahishwa na inonga

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Simba inabidi waangalie mbadala wa huyo jamaa. Ana wenge mno. Kuna moja aliipata Yuko mwenyewe huku mchezaji wa wydad anakuja speed jamaa akaona isiwe kesi, akainyanyua halafu akaipiga kichwa kwenda kwao Ili kipa adake, nilicheka mno
 
Mimi niliona kama vile Shomari Kapombe alipiga kichwa vibaya-katikati ya kichwa ndio maana mpira ukabaki maeneo ya goli na Buli Sambu akapiga kichwa rahisi huku Onyango akishangaa shangaa.

Yote kwa yote. Inabidi Simba watafute mabeki wa kati visiki wanaojua kuruka na kumkaba mshambuliaji. Bila ya hivyo Simba wataishia kuzinyanyasa timu ndogo ndogo tu.

Angalia wale beki watatu wa Wydad. Walikuwa wanacheza kufa na kupona. Walimuweka Baleke kifungoni
 
Hata hivyo namba kumi na moja na namba kumi walitepeta mipira ilikua haimfikii kabisa balleke kwa Hilo huwezi kumlaumu kabisa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwangu Mimi man of the match ni Henock Inonga.
huyu mtu ni "six cylinder" ana sifa za kipekee ambazo hakuna mchezaji wa Simba mwenye nazo..

ni mchezeahaji na pia ni "moderator" anaye jiamini na mchokozi n.k n.k kabarikiwa ...
hiki kifaa inabidi Simba wakinganganie.

naomba kupatiwa utaratibu nimpe sio maua tu bali laki moja akanywe supu.
 
Naam hakika anastahili pongezi [emoji2935]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…