Hawa ni kina nani?

Shabdullah

Member
Joined
Feb 17, 2020
Posts
65
Reaction score
52
HAWA NI KINA NANI???

UZI [emoji116]
Siku za hivyi karibuni utakuwa umekutana na video za hawa jamaa ambao kila mtu amewapa jina lake : wengine wanawaita kamati ya roho mbaya, wengine wajuba na majina mengine mengi. [emoji19]

NI KINA NANI?

Jamaa wanatokea nchini Ghana, ambako ni utamadauni wao kufanya mazishi yakiambatana na sherehe kubwa na kufurahia. Kundi unaloliona linatrend sana siku hizi liliundwa mwaka 2010, kiongozi wao ni Benjamin Aidoo ,ambaye kwa sasa ni star uko Ghana.

Mwaka 2017 Benjamin alifanya mahojiano na *BBS akaeleza kwamba "watu wa Ghana wanathamini sana watu waliokufa kuliko walio hai " yeye aliongeza thamani kwenye biashara yake ya Majeneza , akabuni mitindo ya kucheza, mteja akienda anaambiwa achague anataka mtu wake azikweje, na wengi huwa wanachagua wanapenda watu wao wasindikizwe kwa mbwembwe za kucheza .[emoji116]

Ule wimbo wa (Astrominia) unaotumika kwenye video zao za mtandaoni umeongezwa tu .Lakini nyimbo mbalimbali hutumika msibani.

JAMAA WANAPIGA HELA : Huko Ghana watu wanakopa Bank ili wakafanye sherehe za mazishi ,mtu kununua jeneza la Million 1 hadi 5 ni jambo la kawaida tu [emoji116]

Benjamin Aidoo hutoa huduma zake kwa mtonyo wa Cedis 2,220 ambao ni kama Sh. 883,754 hiyo ni ya kwenda kucheza tu hujaweka ya kununua Jeneza .

#Mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa kazi yao ni kucheza na kuburudisha kwenye msiba huko Ghana wanalipwa more than 800k kwa pesa za madafu...wafiwa hadi wanakopa ili tu wawalipe hawa jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…