Niseme ukweli ninakerwa sana na message za watu wanaojiita patapata. Unafuta inaingia nyingine. Nimejaribu kutafuta namna ya kuwazuia lakini imeshindikana.
Naomba mnipe ushauri nifanye nini au kama TCRA wanaweza kusaidia hili naomba mnisaidie namba yao ya huduma kwa mteja.
Kusema kweli biashara nyingine ni za kihuni na utapeli na bado zinaendelea.
Asee!
Wananchi tuna kazi ngumu sana maana matapeli wengi kama Kalynda huenda wanafadhiliwa na watu wenye dhamana serikalini.
Hii pata pata imekuwa kero sana kwangu
Asee!
Wananchi tuna kazi ngumu sana maana matapeli wengi kama Kalynda huenda wanafadhiliwa na watu wenye dhamana serikalini.
Hii pata pata imekuwa kero sana kwangu
Mimi ilikuwa kwa siku wanatuma hadi meseji 4, niliandika uzi humu. Ikabidi niende offside za tigo kuonba msaada. Kutokana na winging wa meseji za kubeti hadi mtoa huduma alinihurumia.