Hawa Vijana wa kiume kutoboa masikio! Kulikoni?

Hawa Vijana wa kiume kutoboa masikio! Kulikoni?

Freyzem

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
10,120
Reaction score
24,667
Hivi sasa, kumekuwa na tabia inayokua kwa kasi sana inayohusisha vijana wa kiume!Tabia ya vijana hawa ya kutoboa masikio linaweza kuwa moja au yote, kisha kuvaa vipini kama wasichana au kama hajatoboa basi anaweka kipini kwenye sikio moja au yote, inakomaa kwa kiasi kikubwa!
Mara nyingi huu utamaduni tumekuwa tukiuona kwa wenzetu wa huko ng'ambo na kwa watu ambao ni wasanii lakini hivi sasa vijana wa kawaida tu huko mtaani wanafanya hivyo! Hali hii hivi sasa imeanza pia hata kufikisha mizizi yake vijijini tofauti na hapo awali ambapo zaidi ilikuwa mijini!
Imekuwa ni kama kawaida kila vijana 20 basi siyo ajabu utakuta mmoja kavaa kipini kwenye sikio!
Wadau, hebu tujadiliane nini sababu ya vijana wa kiume kuvaa hivi vipini kwenye masikio?
Je kuna ajenda iliyofichwa kwenye hili?
37245461_1858944210885531_1766914107799240704_n~2.jpeg
 
utakuta mkeo kafa na kuzikana na huyo kipini unayemzungumzia na kumleta hapa kwa ma great thinkers.
 
Ulimbukeni na kuiga tu mambo ya hovyo.

Siku wameanza kupaka na rangi kucha.
 
HARUFU sina mizuka ya kutoga masikio.

HARUFU sina mizuka ya kujichora mwili wangu (tattoo).

Naupenda sana mwili wangu
 
Live your life bro don't give shit to someone life
Acha watu wafanye kitu roho inapenda
 
Back
Top Bottom