Ajira za jeshini jw huwa ni mjuano Sana ,watoto wa majenerali ,na masajenti waliostafu ndio wanapita huko Tena kwa simu tu kutoka juu ....
Hizi nyingine polisi ,magereza ,zima Moto ,uhamiaji ,tanapa ndio wengi wanapita kwa ujuzi wao ....japo connection ni mhimu ...
Hao walinzi wa Suma jkt ni watu walioenda jkt wakiwa na malengo ya kuajiriwa polisi ,magereza ,tpdf ,zima Moto n.k lakin walikaa zaidi ya miaka 2 mkataba ukaisha wakafukuzwa kambin na kurudi nyumbani ,,,,kwa vile wanachet Cha jkt ndio wanaomba kuwa walinzi Suma jkt,maana sifa wanakuwa nazo ....ndio maana muda mwingi wako na hasira ,gubu ,ukijichanganya tu wanakuwashia Moto ,maana wako pale kwa bahati mbaya sio lengo lao kabisa [emoji3],,,hata mishahara ni mdogo Sanaa ,stress ni nyingi ,,,maaana wanazidiwa hata na wafanya usafi wa UN ....
Wasameheni bure wale vijana wamepitia mengi Sana ,na kuishi tofauti na matarajio mbaya zaidi hakuna namna nyingi ,wengi utakuta wanavuta Sana sigara ,bangi ,kunywa pombe ,...