Hawa wachina wa Home City walifanya nimkumbuke Kaburu wa Game Sup. Mark

Hawa wachina wa Home City walifanya nimkumbuke Kaburu wa Game Sup. Mark

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
2,254
Reaction score
5,161
Sikumbuki ile siku ilikuwa siku gani kati ya Jumamosi na Jumapili. Nipo na family mwaka jana mwishoni. Tumeenda fanya shopping vitu vya siku kuu.

Tukiwa ndani ukafika muda wa kufunga duka kama sikosei ilikuwa saa 12 jioni. Wahudumu walianza ku harass wateja kuwa either wafanye haraka kununua vitu au wakatishe maana muda umeisha. Hapo tupo ndani. Hili lilinisikitisha sana.

Kule juu tuliambiwa kabisa tushuke na waliokuwa chini wakawa wanazuiliwa kupanda juu kwenda kununua vitu acha kufanua window shopping. Wale macho kuvimba wapo tu wanaangalia wateja wanakuwa harrassed wala hawashtuki. Mteja anafokewa kuwa inatosha sasa aondoke duka linafungwa.

Kama wangefunga gate watu wasiingie inaeleweka na ni sawa .lakini kuwabalasa wateja walioko ndani watoke ilikuwa very unbecoming. Ilileta picha mbaya sana. Hakukuwa na customer care tena.

Nikakumbuka mwaka flani nikiwa game nlikutwa na jambo kama hilo nikiwa ndani. Muda wa kufunga umefika. Kaburu alinifuata nikiwa na watoto nawaharakisha tutoke. Akaniambia No. Sir just relax let them enjoy we are here for you. Mswahili mmoja alinikata jicho. Yule Mzungu alikuja akawa anazunguka nasi anamsukuma mtoto wangu kwenye toroli.

Nikakumbuka siku moja nimenunua kitu flani chakula watoto kumbe bei imechanganywa. Kale kamfuko ka kilo 1 tu it was tsh 19,000. Nikachukua vinne nikidhani ni tsh 1,900. Nikiwa nalipia pale nakuta jumla imekuja ya kutisha maana mimi huwa nakodolea macho nikisia tii naangalia. Nikamwambia mhusika hii bei hapana. Mifuko minne tsh 76,000 haukamu? Ndo akasema kimoja ni tsh 19,000.

Nikasema no wei ondoa hiyo kitu. Si unajua yale maeneo inabidi ujue maneno mawili matatu ya kizungu. Akasema anamwita boss wake aje afanye kitu.

Akaja kaburu.akaelezwa. akasema haina shida ngoja kwanza akaangalie. Kwenda kule akarudi akasema ni kweli waliobandika price wamekosea. So nipewe kwa bei hiyo ya Tsh 1,900. ila bei zake ni tsh 19,000. Nikakataa kuwa aiondoe tu. Akasema no.nipewa mimi nipo sahihi wao wamekosea si kosa langu. Aiseee....sikuweza sahau ule ukarimu wa kibiashara wa wale makaburu.
 
Kuna siku nilivaa ndala, aisee wale Suma jkt walijua ni chizi. Yaani kidogo wanizuie. Walivyojaribu kuniongelesha ndyo wakaamini kwamba nimependa tu kuvaa vile.

Mchina akikaa pale ndani upande wa kushoto hanaga muda hata wa kugeuka, nahisi ni kamera zinamdanganya kwamba ataona Kila kitu on the spot kwenye screen
 
Kwa bahati mbaya kaburu unae mzungumzia kama ni WA game ya mlimani city...alifanyiwa figisu figisu Hadi akatoroka kama mkimbizi...wabongo linapokuja swala la upigaji wapo teyari kufanya chochote​
Naskia watu wa shoprite mataifa mengine huko kusini hawataki kuwasikia watanzania kabisa. Mtanzania yoyote akiomba kazi hapewi kwenye chain zao kwasababu ya upigaji. Unaambiwa shoprite na uchumi bongo wafanyakazi walikuwa wanawaita ndugu zao na marafiki kufanya shopping na kuwaelekeza kupita counter bila kulipa. Wamefanya hivyo muda mrefu hadi kaburu kuja kushtuka akaweka mlinzi kila counter ukishalipia mlinzi anaikagua risiti na kustump muhuri.

Mbongo kwa upigaji ni hatarii.

Yoda mrangi mshamba_hachekwi min -me

Nyau de adriz
 
Kwa bahati mbaya kaburu unae mzungumzia kama ni WA game ya mlimani city...alifanyiwa figisu figisu Hadi akatoroka kama mkimbizi...wabongo linapokuja swala la upigaji wapo teyari kufanya chochote​
Sisi waswahili tunapenda ubabaifu sana aiseee.... Game walikuwa na vitu quality kwa bei rahisi.
 
Kuna siku nilivaa ndala, aisee wale Suma jkt walijua ni chizi. Yaani kidogo wanizuie. Walivyojaribu kuniongelesha ndyo wakaamini kwamba nimependa tu kuvaa vile.

Mchina akikaa pale ndani upande wa kushoto hanaga muda hata wa kugeuka, nahisi ni kamera zinamdanganya kwamba ataona Kila kitu on the spot kwenye screen
Wachina hawana customer care pia. Wakali sana... Afadhali hata wahindi.
 
Wachina hawana customer care pia. Wakali sana... Afadhali hata wahindi.
Acha wawe hivyo, wasipokuwa hivyo mbongo ana mazoea mabaya sana anataka hadi akurukie mabegani humo dukani.

Ndo maana 'teeth' wamezidisha utekaji isingekuwa hivyo watu wangekuwa wanajisaidia hadharani getini magogoni.

Mbongo ukimuendekeza ana mazoea mabaya sana.

Nyau de adriz
 
Mkuu ni kwasababu wameshajua tabia mbofumbofu ya mbongo ya wizi. Hata Ghetto tu ukimkaribisha mbongo ataliza nail cutter na flash
Yaani Kuna muda unaona kabisa wanajaribu kama wateja wa aina fulani ndyo wanatakiwa kupata huduma pale.

Wanazingatia physical appearance utadhani tunaenda kuomba kazi, shenzi kabisa
 
Naskia watu wa shoprite mataifa mengine huko kusini hawataki kuwasikia watanzania kabisa. Mtanzania yoyote akiomba kazi hapewi kwenye chain zao kwasababu ya upigaji. Unaambiwa shoprite na uchumi bongo wafanyakazi walikuwa wanawaita ndugu zao na marafiki kufanya shopping na kuwaelekeza kupita counter bila kulipa. Wamefanya hivyo muda mrefu hadi kaburu kuja kushtuka akaweka mlinzi kila counter ukishalipia mlinzi anaikagua risiti na kustump muhuri.

Mbongo kwa upigaji ni hatarii.

Yoda mrangi mshamba_hachekwi min -me

Nyau de adriz
nabisha aisee

mbona walisepa kenya pia?

watu maskini wanaamini vitu vya mtaani kuliko supermarket

ndo maana retailers wanaofanikiwa huku ni wa fashion na dawa tu(little more, vunjabei)

ukishaleta mambo ya vyakula, furnture nk wabongo utawakosa
 
Naskia watu wa shoprite mataifa mengine huko kusini hawataki kuwasikia watanzania kabisa. Mtanzania yoyote akiomba kazi hapewi kwenye chain zao kwasababu ya upigaji. Unaambiwa shoprite na uchumi bongo wafanyakazi walikuwa wanawaita ndugu zao na marafiki kufanya shopping na kuwaelekeza kupita counter bila kulipa. Wamefanya hivyo muda mrefu hadi kaburu kuja kushtuka akaweka mlinzi kila counter ukishalipia mlinzi anaikagua risiti na kustump muhuri.

Mbongo kwa upigaji ni hatarii.

Yoda mrangi mshamba_hachekwi min -me

Nyau de adriz
Mkuu nimecheka sana, mbongo hatari sana kwenye kuiba 😃
 
Okay! Home City ni Supermarket ya bidhaa mbalimbali (kasoro vyakula na vinywaji) inayomilikiwa na Wachina ipo Mlimani City upande wa Mlimani Conference Halls.
PXL_20250130_055717755.jpg
 
Back
Top Bottom