Hawa Waha wanaokopesha vyombo ni wachawi kweli kweli

Ivi kwanini mtu anakua na roho ya utapeli,kwanini mtu anachukua kitu Cha mtu unajua kabisa sitomlipa.

Aisee tubadilike.
Kulipa ni ngumu unapojua unatapeliwa kitu cha elf20 dukani yeye anataka akupige 50
 
Kuna mama mmoja hpa kitaa deni lilikuwa kubwa akataka akimbie, ile siku ya kuhama Muha amefika ngoma ikaenda hadi kwa mjumbe ikabidi wagawane vyombo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Acheni dhulma watu wenyewe wamechoka vile anatembeza vyombo kutoka Mbezi mpaka Mbagala bado unataka kumdhulmu?? Kwano amekulazimisha kukopa?
 
Hiyo , Biashara ngumu lakini faida inapatikana Katika kuuza kitu Cha 10k anauza 30 kwa mkopo so probably kila siku akizikusanya bukubuku hizo Kuna Faida atatengeneza mwisho wa mwezi ,
Wengi kupitia Kazi hii wamewekeza kwao kigoma na baadhi wameenda extra miles kwa kumega wake za watu. Na kudhulumia na mwisho kurudi kigoma
 
Yaani mwanaume anatoka nyumbani,,, anaacha mke mjamzito anakuja kutafuta hela dar mpaka mke anajifungua mtoto anafikisha miaka 2 bado anatafuta ili apate chochote cha kurud nacho alafu wewe unakopa chombo chake unamzungusha na matusi juu,,,, yaani kwa uchungu alionao anaweza akakutamkia na laana ikawa juu yako sio mpaka uchawi!!! Heshim jasho la mtu
 
Deni dawa yake rejesho
 
Acheni dhulma watu wenyewe wamechoka vile anatembeza vyombo kutoka Mbezi mpaka Mbagala bado unataka kumdhulmu?? Kwano amekulazimisha kukopa?
Wewe unazungumzia wamachinga, Hakuna muha aliechoka huku
 
Kuna mama mmoja hpa kitaa deni lilikuwa kubwa akataka akimbie, ile siku ya kuhama Muha amefika ngoma ikaenda hadi kwa mjumbe ikabidi wagawane vyombo
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]nawaogopaga sijawahi kopa kwao maana vitu vyao maana Bei zao ghalii mnoo mara mbili au tatu ya mjini
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]nawaogopaga sijawahi kopa kwao maana vitu vyao maana Bei zao ghalii mnoo mara mbili au tatu ya mjini
Na ukiingia huo mtego utoki bora ukatae mapema
 
Umekutana na kiboko ya dhulumati
 
Daah hawa jamaa najiuliza wanapataje hela
Hawa watu wanakiwango kikubwa sana Cha uvumilivu.
Kwa mfano amenunua kitu kwa sh elfu 5. Yeye anakopesha elfu 10. Lkn anakuwa anapewa bukubuku. So unakuta mteja anatoa buku leo. Mara kesho atajifanya Hana,
kesho kutwa tena akimuona muha atajificha ndani watoto wanasema mama hayupo. Kwa hiyo unakuta hiyo elfu kumi inaenda Hadi mwezi kukamilika.
Hawagana hata hasira pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…