Hawa wanaojiita mawakala wa TRA wanauza electronic EFD Machines wanatoa wapi namba zetu?

Hawa wanaojiita mawakala wa TRA wanauza electronic EFD Machines wanatoa wapi namba zetu?

Joined
Jun 26, 2024
Posts
16
Reaction score
16
Kumekua na tabia za kupigiwa simu na watu wanaojiita mawakala wa TRA wakitangaza biashara zao za kuuza electronic efd machines kwamba unaweza kutoa efd receipt kupitia simu ya mkononi. Natambua kwamba hilo linawezekana lakini, swali langu ni kwamba wanatoa wapi hizi namba zetu? na wanajitambulisha kama mawakala wa TRA. Je TRA wametoa jukumu hilo kwa haya makampuni, na kama ni kweli, TRA wametoa wapi kibali cha kugawa namba za watu kwa haya makampuni bila kumshirikisha mhusika.

Nimeshapigiwa simu na makampuni mawili tofauti wanajitangaza na kujitambulisha kama mawakala wa TRA, ukiwauliza wametoa wapi namba wanasema wamepata namba za wafanyabiashara, nikawauliza hizo taarifa zenu zinaonyesha mi nafanya biashara gani hawajui. Sasa naomba TRA watoe tamko kama siku hizi wana mawakala wa kuuza efd machines na hizi namba zetu wamezigawa za nini bila kuomba ridhaa yetu. Wasije wakawa wanauza taarifa zetu na kujipigia pesa.

TRA toeni tamko ili tujue kama kuna uhalali wa hawa watu au tuwapeleke polisi, na pia kama mnawatambua mtuambie ni lini sisi tulikubali mgawe namba zetu kwa haya makampuni yenu.
Mkumbuke Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inazungumzia utunzaji wa taarifa binafsi lakini pia inasisitiza swala la ridhaa kwa mmiliki wa taarifa binafsi kabla ya kuchakata au kusambaza taarifa zake. Sheria hii haichagui Taasisi ya Umma wala Binafsi, wote wanatakiwa kuifata.
 
TRA awawezi kumpa mtu yeyote taarifa zako...! Kwasababu hata wao wenyewe tra taarifa zako Awana😂😂😂 kwani ndugu muandishi Tra weshawahi kukupigia simu..?

Kwa kifupi hao mabwana mawasiliano Yako wameyatoa humu mitandaoni ambako una sign in kutumia either email Yako au namba zako za simu...!

Simu zetu hizi zinatunza taarifa za mambo tunayo yasoma na kuyatizama mara kwa mara mitandaoni...hicho ndicho kinacho wavutia wenye matangazo yao Hadi wanakufahamu kuwa wewe ni mfanyabiashara ambae Wana kuhitaji...!​
 
Wewe ndo huelewi kitu mkuu.

TRA ndo wanaotoa hizo info zako,na baadhi ndo wamiliki wa hizo kampuni
 
Back
Top Bottom