Hawa wanaweza kuoana?

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,891
Wazazi wa vijana hawa wawili wanaishi pamoja kama mume na mke,na wameishi hivyo kwa miaka mitano,lakini wote wawili wana umri mkubwa,baba 52 mama 50,wakati wanakutana wote walikuwa na watoto hawa kabla,watoto hawa walifahamiana na kuanzisha mahusiano baada ya wazazi wao kuwa pamoja binti ana miaka 25 na kijana ana 29,binti ndo alianzisha uhusiano kwa kumwambia kijana hisia zake,kijana akawa mgumu kutokana wazazi wake,lakini baada ya muda kupita akawa amekubaliana na binti,sasa wanajiuliza kama wanaweza kufunga ndoa kwani uhusiano wa gf na bf sio sawa na ndoa,ndoa ni kubwa zaidi,kabla hawajalipeleka jambo hili kwa wazazi wanaomba ushauri,alielileta kwangu ni kijana ambae ni rafiki yangu na pia ni alikuwa mfanyakazi mwenzangu!Nitashukuru kwa maoni na mitazamo yote!Je wanaweza kuoana wakati wazazi wao ni wanandoa?Kumbuka hawa hawajashare mzazi hata mmoja,mama wa binti na baba wa kijana waliwapata hawa watoto wao kabla hawajawa pamoja!
 
kama tayari wanafanya hayo mambo hakuna tofauti na wakioana.
 
Google incest, pia some Penal Code (kanuni ya adhabu kwa makosa ya jinai) ya Tanzania, kisha uje tena hapa kuuliza swali lako. Sawa sawa?
 
Google incest, pia some Penal Code (kanuni ya adhabu kwa makosa ya jinai) ya Tanzania, kisha uje tena hapa kuuliza swali lako. Sawa sawa?


mkuu hio hai qualify kuitwa incest.
 
kwa ushauri,kama mioyo yao imeridhiana na wakavuliana vigagula kuna haja gani ya ushauri?


Mbona wanaweza oana mana hawajashare damu.ingaw wazazi wao wanamahusiano.

Je wangekua hawaishi pamoja na maanisha wazazi,c ingekua rahisi kwao kutangaza NDOA?

Wasonge mbele na mausiano.
Sasa cjui mama mkwe ataitwaje mana mwanzo alikua anamchukulia kama mama,na BA MKWE sijui ataitwaje mana mwanzoni alikua anaitwa Baba.
 
Kwa mtazamo wangu....... kitendo cha wazazi wao kuwa pamoja kimewafanya wao kuwa kaka na dada................walichokifanya hakina heshima
 
hali unayokua nayo unapokua katika hali ambayo hauko relaxed na wajilazimisha kuonesha uko.
Thanx,naona wewe ni mwalimu,but sikuwa katika hali hiyo!
 



sasa umeongea.
 
Kwa mtazamo wangu....... kitendo cha wazazi wao kuwa pamoja kimewafanya wao kuwa kaka na dada................walichokifanya hakina heshima
Kaka na dada wa ukubwani sio ki biological. Nadhani atangaze ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…