SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,265
Ni Bernard James na Sauda Mwilima wote watangazaji wa Star Tv. Bernard James wakati mwingine anatangaza michezo na Sauda siku zote ni kipindi cha Bongo Beats. Wote wawili wanapenda sana kutumia neno 'kuweza' na wanalitumia kwa namna ambayo si sahihi (Nionavyo mimi)
Kwa mfano, Bernard James akitangaza mchezo wa mpira wa miguu utamsikia akisema: " Taifa Stars iliweza kufungwa mabao 4 na Ivory Coast. Neno hili la 'kuweza' anapenda sana kulitumia.Naye Sauda Mwilima kwenye wasifu wa mwana hip-hop aliyezikwa hivi karibuni alisema: " Mwanamuziki Langa aliweza kuugua na kupelekwa Muhimbili kwa matibabu. Huko basi, mambo yalishindikana na akaweza kufariki"
Je, wataalamu wangu wa lugha, hayo ni matumizi sahihi ya neno 'kuweza'?
Naomba msaada.