Hawa watu wawili (2) walizaliwa hapa Tanganyika/Tanzania nyakati zisizo sahihi kwao!

Hawa watu wawili (2) walizaliwa hapa Tanganyika/Tanzania nyakati zisizo sahihi kwao!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2016
Posts
1,770
Reaction score
5,423
1. Mwl. Julius Kambarage Nyerere

Ukitazama akili, ushawishi na maarifa aliyokuwa nayo ingepaswa azaliwe kipindi ambacho nchi inao wasomi wa kutosha kumpa changamoto. Waliokuwepo wachache kama akina Hayati Kambona lakini kwa nchi kutokuwa na wasomi akina Hayati Kambona waliishia kuonwa wasaliti.

2. Zitto Zuberi Kabwe

Huyu anapambana kipindi ambacho tuna watu wanaojidai wasomi lakini wengi ni wachumia tumbo tu! Wasomi wa aina ya akina Mwigulu Nchemba, Palamagamba Kabudi n.k.
 
4. Chifu Mkwawa.
Aliweza kupambana na wakoloni miaka hiyo. Alitakiwa aishi enzi za TANU na angefaa kuws Rais wa kwanza wa Tanganyika na Tanzania. Pamoja hakuwa msomi na hakuenda hata darasa moja ila alikuwa na akili sana. Kama angekuwa enzi za TANU nchi na akawa Rais nchi ingekuwa mbali sana.
 
Ni kweli kabisa, tena huyo wa kwanza hakustahili kabisa kuwepo tz, maana baada ya kutengeneza na kuitumia katiba ya nchi zaidi ya miaka ishirini, tena baada ya kutoka madarakani ndio anakuja kusema hii katiba inchi ikipata rais kichaa anaweza kuwa dictotor, hongera kwa bandiko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3. Mch Mtikila.
Aliipigania demokrasia yeye peke yake wengine tukamuona mwehu.
Alifanikisha swala la mgombea binafsi kwenye nafas ya urais
Kwa hiyo mgombea binafsi upande wa rais ruksa tangu lini?
 
Mleta mada nakushauri kimbilia mirembe kwani una dalili zote za mwendawazimu, ujinga wa kiwango cha lami ulichoandika!
 
Ninachojua ni kwamba hii ni vita kati ya wanaotawala na wanaotamani kutawala. Nyerere alichua nafasi ya wazungu kwa niaba ya waswahili wenzake, Zito kabwe anapambana ili achukue nafasi iliyoshikwa na waswahili wenzake. Ina maana anagombania zamu ya kutawala, sasa hapo ndipo tafsiri ya mtu kuitwa shujaa inaposumbua..
 
humu kuna watu wanajikuta wajuaji sana wa mambo kumbe hata pengine wanashindwa kuyadadafua katika maisha yao ya kila siku.mfano wa Nyerere kuzaliwa katika wasomi wachache ni sawa useme kina Mao ,Mahindra,Kenyattah,Nkurumah pia walizaliwa kwenye wasomi wachache kana kwamba uongozi ungewashinda katika hali ya sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom