Dr wa Manesi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2024
- 997
- 1,220
Kumchelile? Kwali mwenga!
Kila nikipita humu JF lazima nikutane na Uzi unazungumzia ukatili wa mwarabu. Miaka yangu yote ya kuperuzi humu jf imekuwa hivyo. Na zaidi ni kwa namna gani waarabu wanawachukia, wanawatenga na wanawatesa watu weusi. Nikajikuta nikiwa muumini wa Imani hiyo miaka yote. Na nikifuatilia jinsi wanavyotwangana huko mashariki ya kati Imani yangu ikaongezeka maradufu, yaani nikajua hakuna utu kabisa huko, mtu mweusi ndo takataka kabsaaaa!!
Likaja kombe la Dunia 2022 ambalo lilifanyika huko Qatar, nikiri kuwa katika mashindano yote ya kombe la dunia, hili ndo nililifuatilia vizuri zaidi.........lilinikuta likizo, nikiwa sidaiwi Huku nikiwa na shauku ya kuona hawa waarabu wanaandaaje kombe la Dunia la football badala ya uimbaji wa qaswida. Yafuatayo yalinishangaza huko;
-timu nyingi za nchi za kiarabu (niseme zilizoshiriki kombe la Dunia ,aana nyingine sijaziona) zimejaa wachezaji weusi.....tiiii.
- kamera za uwanjani zilipoonyesha mashabiki wao nilishangaa kuwaona makumi ya mashabiki weusi wakiwa katikati wanashangilia pamoja. Ni kama sikiwa naamini hivi nami nilishameza.
Mara Ronaldo anahama man u na kwenda huko Uarabuni, hii ikapelekea ligi ya huko kupata umaarufu na kuanza kuonyeshwa. Nami, nikiwa shabiki mkubwa wa huyo mwamba, nikaanza kuifuatilia ligi hiyo iliyoanza kuonyeshwa na king'amuzi changu maridadi Cha muda wote, startimes. Huko nilishangaa zaidi kuona wachezaji na mashabiki weusi kibao majukwaani wakishangilia timu zao. Nikazidi kupatwa na mshangao. Sijaona mweusi hata mmoja Argentina au Uruguay au Japan ila sijawahi kumsikia habari za kuwatesa Wala kuwatenga watu weusi zikisemwa dhidi yao.
Wajuzi na mliotembea na msio na upande, hebu niwekeni sawa kidogo nami nopate elimu......lipi ni lipi?
Ahsanteni.