'Hawakwepi tutawaadhibu tu'' - Rais UEFA

the numb 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2020
Posts
1,562
Reaction score
2,902
Rais wa shirikisho la soka Ulaya 'UEFA' Aleksander Ceferin amethibitisha vilabu vyote 12 vilivyotaka kushiriki mashindano mapya ya 'European Super League' vitaadhibiwa.




''Pamoja na mpango wao kutokufanikiwa, sisi kama shirikisho hatutakaa kimya tutawafundisha somo jipya kwa kuwaadhibu, ukiachilia mbali adhabu wanayoipata kutoka kwa mashabiki wao kwa maandamano na mabango kupinga jambo hili nasi hatutoacha kutoa yetu,'' alisema Ceferin.

Aliongeza, ''hatutataka kujua nani alikuwa kinara wa mpango huu, wala nani alikuwa wa kwanza kujiondoa katika jambo hili, hivyo tutashusha rungu kwa wote.''

Alipodadisiwa juu ya aina ya adhabu wanazotarajia kuzitoa alisema, ''hili litajadiliwa kwa kina japo kwa upande wa Uingereza huenda ikazidi kwa kuwa ilihusisha vurugu za mashabiki kupinga jambo hili japo nadhani haitaenda mbali na adhabu ya faini.''

Majuzi iliibuka taharuki kubwa sana juu ya kuanza kwa mashindano mapya ya ' European Super League' ambayo yalitafsiriwa yanakuja kukinzana na mashindano yaliyo chini ya UEFA kwa kuwa vilabu vyote vilivyotangaza kushiriki huwa vinacheza michuano hiyo.

Vilabu vya Manchester United, Manchester City, Arsenal, Chelsea, Liverpool na Tottenham kutoka Uingereza Juventus, Inter Milan na AC Milan kutoka Italy, Barcelona Atletico Madrid na Real Madrid kutoka Uhispania vilithibitisha kushiriki.
 
Reactions: OIN
Kwa uingereza wanasema huenda adhabu ikawa ndogo sababu walijitoa mapema.
Nafikiri wanataka kutumia mfumo wa divide and rule, wameruhusu matumizi makubwa ya fedha lakini wameshindwa kulinda vilabu vikubwa.
Mawakala kama Raiola wamekuwa wakivikamua pesa ndefu vilabu hivi bila.kujali mzigo unaobebwa na vilabu
 
Watoe adhabu zote ila sio kushusha daraja

Wakiwashuha basi super league insrejea
 
Jamaa nae anataka sifa tu hajua kama hizo team ndio zimeshikilia ugali wake na zikiamua kweli kujitoa zinaweza fanya hivyo. Aache mboyoyo wenzake washakubali kujirudi nae akitulize sasa
Zinajitoa zinaenda wapi?
 
Jamaa nae anataka sifa tu hajua kama hizo team ndio zimeshikilia ugali wake na zikiamua kweli kujitoa zinaweza fanya hivyo. Aache mboyoyo wenzake washakubali kujirudi nae akitulize sasa
Amini super league itarudi na kuchezwa. Humu JF huwa nawaambia sana kuwa hakuna kitu kigumu kama kutengeneza faida kwenye sports industry. Mwezi huu man city wamereport loss ya paund milioni 137 kwa mwaka uliopita, leicester 37, barca wana deni la Euro bilioni 1, deportivo ipo sijui daraja la 4 na madeni yasiyolipika.
Barca na madrid bado wamo super league, rais wa madrid juzi amesema bila sl huwezi kusajili mtu kama neymar, mbape, haaland na masuper star wengine.
JP Morgan wanatoa euro billion 5.4 kwa mwaka, kinachokuja ni kuanzishwa shirikisho lingine la soka mbadala wa uefa na fifa na ligi bora ulimwenguni itapigwa.
Wasiotaka hii ligi ni mashabiki na wanyonyaji wasio na uwekezaji kwenye hii timu
 
UEFA haitaweza kupambana na hao giants. Kwanza hawana legal foundations za kuwaadhibu au ku sue kwa chochote.

Hii battle ikitokea UEFA watakuwa kwenye upande wa kupoteza.
 
Kwanza wajiulize!! Kwanini hivyo vilabu vilianzisha hiyo ligi yao? Je hii ligi ya sasa ina mapungufu yapi?
 
Juventus na arsenal ilibidi ndio wagangamale kweli na ESL.. maana mara kibao wametolewa kafara ili timu pendwa za uefa(bingwa mtarajiwa) abebe kombe
 
Nimeangalia jina lako,na hiyo avatar [emoji23][emoji23][emoji23]sana.
Iyo league aseno na spurs wangeshuka daraja......


Perez ndio akubali rasmi sasa soka la ulaya limeshikiliwa na england watakachokiamua wao hakuna wa kuwapinga.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…