Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mufti Sheikh Hassan bin Ameir
Katika masheikh waliosomesha Tanganyika Mufti Sheikh Hassan bin Ameir ameacha historia ya pekee kabisa.
Licha ya kuwa Ulamaa mkubwa wa kutegemewa alikuwa pia mpigania uhuru na mmoja wa wanachama wa mwanzo wa TANU.
Sheikh Hassan bin Ameir anakumbukwa kwa kuuza kadi za TANU katika misikiti yote aliyokuwa akipita kudarsisha na kuwahimiza Waislam kujiunga na TANU kupigania uhuru.
Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa mjumbe wa TAA Political Subcommitee (Kamati ya Siasa ya TAA) iliyowajumuisha Dr. Vedasto Kyaruzi (President), Abdulwahid Sykes (Secretary), Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Steven Mhando na John Rupia.
Kamati hii iliundwa mwaka wa 1950.
Kamati hii ndiyo iliyoandika na kuwasilisha mapendekezo kwa Kamati ya Gavana kuhusu Katiba ya Tanganyika maarufu kwa jina la Constitional Development Committee iliyoundwa na Gavana Edward Francis Twining.
TAA Political Subcommitee ilipendekeza wajumbe katika LEGCO wachaguliwe kwa kura moja mtu mmoja badala ya kuwa wanateuliwa na Gavana.
Halikadhalika walipendekeza kuwa baada ya kutimiza hilo mwaka wa 13 Waingereza waondoke Tanganyika.
Mapendekezo haya yaliwaudhi Waingereza kiasi waliamua kuwaondoa viongozi wote wa TAA Dar es Salaam na kuwapeka majimboni mbali sana na Dar es Salaam ili kuua harakati za kudai uhuru.
Hamza Mwapachu alijikuta yuko kisiwani Nansio Ukerewe.
Dr. Vedasto Kyaruzi alipelekwa Kingolwira kisha Nzega.
Abdul Sykes chupu chupu aondolewe katika nafasi ya Market Master Soko la Kariakoo.
Waraka huu ulijadiliwa katika mkutano wa kuasisi TANU mwaka wa 1954.
Itoshe tu kuwa hotuba aliyosoma Julius Nyerere UNO mwaka wa 1955 inatoka katika waraka huu.
Katika nyaraka muhimu zilizopotea na hazijulikani zilipo hadi leo ni waraka huu ambao ulisainiwa na Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na wajumbe hao wote.
Hakika ni waraka wa historia na kumbukumbu kubwa sana.
Waraka huu umapata kusomwa wote na Cranford Pratt muasisi wa Kivukoni College na kausifia pakubwa katika kitabu chake, ''Critical Phase in Tanzania 1945 - 1968.''
Baada ya miaka mingi toka Sheikh Hassan bin Ameir kufariki Zanzibar mwaka wa 1979 hii ndiyo mara ya kwanza kusikia kakumbukwa na kafanyiwa hawli.
Inahitaji kitabu kizima kueleza historia ya Sheikh Hassan bin Ameir:
View: https://youtu.be/Fs6rsPAhrbA