Haya CHADEMA njooni Tusemezane. Wala haina haja ya kupapasana mgongoni Ukweli ni Upi?

Haya CHADEMA njooni Tusemezane. Wala haina haja ya kupapasana mgongoni Ukweli ni Upi?

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Karibuni weekend nadhani ipo njema kabisa. Sasa ,mimi nimewaita kwa issue moja tu muhimu. Msikasirike sisi watu wenye Ubara ndani yetu huwa hatujui kuuma uma maneno.

Nyie Watanzania wenzangu inakuaje mpaka sasa Zaidi ya Miaka 15 hamwoni haja ya kujenga Ofisi ya Makao Makuu?Mnaogopa nini?

Ni kama hamjiamini na mnajua siku yoyote chama kitakufa. Maana kama si hivyo mlikuwa na uwezo wa kujenga ofisi ya chama kubwa ya kisasa kabisa. Pengine wasiwasi ni kuwa chama si cha kudumu je mkijenga jengo litakuwa la nani ikitokea mwenyekiti ameondoka.

Kwa sasa Chadema kinakosa watu wenye akili watu wazima kama akina Prof Safari, Baregu. Ukimtoa Tundu Lissu unabaki na akina nani? Hilder?

Jengeni ofisi bwana kila siku mnaonekana wahuni. Ni sawa na kijana ambaye hataki kujenga, haoni haja maana ameshapima amekutwa ana ngoma au kansa. So anasema ajenge ili iweje? wacha ale maisha. Amekata tamaa.

Mi nawaambia ukweli hata kama mta mind. Ukweli ni upi? Mnakula pesa za chama/ruzuku? Hamjiamini kudumu muda mrefu? Wahuni na walaji ni wengi?mwenyekiti hajaona umuhimu wa kujenga sababu wasiwasi ni mkubwa?

Nimekaa pale 👉
 
CCM ina ofisi kila Kata lakini ndicho chama kilichojaza wala rushwa, watoa rushwa, wagandamizaji, wezi wa mali ya Umma, watengeneza dawa feki za ARV, wakwepa kodi, watu wenye udini, ukabila, na walaji wakubwa wa kodi za watanzania bila ya kufanya kazi ya kujenga nchi.
 
Suala la ofisi zao mimi hata halinisumbui.. Kinachonisumbua mimi ni mtu watakayetuletea kuwatoa CCM madarakani.. Watuletee mtu sahihi Tuwafurahishe CCM..
 
Taifa linakosa Nishati ya umeme ,Maji hayatoki wewe unaongelea ofisi za chadema.utakuwa umetumwa kwani nyumbani kwako ukiwa na nyumba nzuri na jirani yako anaishi kwenye slope utamdharau?? Kipi Bora kuwa masikini wa halali au tajiri wa kuua watu,kupora haki ,kupora uchaguzi, ufisadi,wizi,utapeli na MIKONO yenye DAMU chagua mwenyewe utakaa kundi gani??
 
Unawaza ofisi za Chadema, wakati watoto wanakaa chini madarasani hawana madawati,wanasomea chini ya mti hawana majengo.

Miaka zaidi ya 60 ya uhuru mpo madarakani bado Maji safi ni tatizo, mmeshindwa kupambana na adui Maradhi na Ujinga mnapambana na Chadema.
 
Lame excuse. Jengeni ofisi muonekane mpo serious. Siyo kugawana ruzuku tu.
 
Naunga mkono hoja inakuwaje chama kikuu Cha upinzani kishindwe kujennga ofisi,Ruzuku inaenda wapi?mnakatisha tamaa sna, chama kinawanachama wengi sna Kwa nn msiitishe wanachama tuchangie? Mwenyekiti hili jambo lifikirie xna, na ww ujitoe Kwa ajili ya watazania
 
CCM ina ofisi kila Kata lakini ndicho chama kilichojaza wala rushwa, watoa rushwa, wagandamizaji, wezi wa mali ya Umma, watengeneza dawa feki za ARV, wakwepa kodi, watu wenye udini, ukabila, na walaji wakubwa wa kodi za watanzania bila ya kufanya kazi ya kujenga nchi.
Duh !
 
Back
Top Bottom