SoC03 Haya huishia katika maadhimisho?

SoC03 Haya huishia katika maadhimisho?

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
May 24, 2016
Posts
15
Reaction score
10
Ili maisha bora yaendelee kila kiumbe kinchopumua kinahitaji chakula kwanza ndipo mambo mengine yaweze kuendelea. Lakini siyo chakula tu bali inahitajika kutambua kwanza usalama wa hicho chakula na ubora wake ndipo uweze kukitumia kwa uhakika wa kukupa nguvu na afya ya kuendelea kuujenga mwili, kuulinda na kuukuza kwa kadiri ya umri wa hicho kiumbe.

Katika makala hii tunaenda kujadiliana kuhusiana na maadhimisho ya usalama wa chakula Dunia inayofanyika Juni 7 mwaka huu na hufanyika kila mwaka, ambapo mwaka huu katika kuelekea siku hiyo kuna mambo yalizungumzwa ili yawafikie wanachi waweze kuyafanya ili kufikia lengo la usalama wa chakula.

Lakini pia tutajadilia mambo yaliyojitokeza katika siku ya maadhimisho hayo Duniani kote ambayo mwaka huu yalikuwa na kauli mbiu "viwango vya chakula huokoa maisha."

Hapa nchini katika kuelekea siku ya maadhimisho hayo Mei 25, 2023, Kaimu meneja wa kitengo cha tathimini ya vihatarishi vya chakula kutoka katika shirika la viwango Tanzania (TBS), Dkt.Ashura Kilewela, alizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na viwango vya chakula vinavyotakiwa wananchi wavijue ili katika kuandaa wahakikishe wanafikia hivyo viwango.

Ili kupunguza hatari kwa jamii kutumia vyakula visivyo na viwango muhimu kwa ajili ya afya ya miili yao. Amesema Shirika la viwango Tanzania (TBS) limeitaka jamii kuzingatia kiwango kinachoelekeza kipimo cha chakula katika ufungashaji na kuwasihi watumiaji wa vyakula kuzingatia maelekezo ya utumiaji wa chakula husika ambayo sana sana hupatikana katika vifungashio.

Amesema, TBS inawakumbusha wanachi kutumia chakula salama hasa katika uzingatiaji katika uandaaji wanatakiwa kutumia malighafi safi na bora pamoja na utunzaji wa chakula. Akizungumza na waandishi hao akiwa jijini Dar Es Salaam, amesema viwango vya uhakika huokoa maisha na ni muhimu katika maisha ya watu ya kila siku, hivyo basi tunatakiwa tuhakikishe tunatumia chakula salama kujenga na kulinda afya zetu.

"Uandaaji wa chakula salama ni jukumu letu sote, kwahiyo ili tuwe na chakula salama kila mmoja anatakiwa kutumia kiwango kile kinachotakiwa." Amesema.

Amesema, maadhimisho ya mwaka huu TBS inategemea kuwashirikisha wananchi na wadau mbalimbali katika kusherehekea kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa matumizi ya chakula salama.

"Lengo la maadhimisho haya ni kuinua uelewa wa jamii juu ya chakula salama, kwasababu ukila chakula salama utakuwa na afya bora na utaweza kufanya majukumu yako ya kila siku kwa uzuri na uhakika zaidi." Amesema Kilewela.

Amesema kwahiyo wanapoelimisha jamii wanasaidia kuepukana na madhara yanayopatikana kwa ulaji wa chakula kisicho salama. Pia kuna kuepuka mambo mengi yanayoweza kutokea kwa jamii kutokujua hatari iliyomo katika kutumia chakula kisicho salama.

Kwa upande wa shirika la afya la Dunia WHO na la chakula FAO, katika siku ya maadhmisho hayo Juni 7, 2023, ambao pia ndiyo huibeba siku hiyo kwa lengo kubwa la kuongeza habari na taarifa kuhusu hatari ya sumu ya chakula na uchafuzi, ambayo inaua watu 420,000 kila mwaka.

Huku vifo 125,000 miongoni mwao vikiwa ni vya watoto wa umri wa chini ya miaka mitano. Na takwimu za mashirika hayo zinaonyesha kuwa kila mwaka kuna angalau kesi 600,000 za magonjwa yanayosababishwa na chakula ambacho huandaliwa bila kuzingatia viwango vya usalama wa chakula.

Pia mashirika hayo yamesema kuwa watu wanaishi katika ufukara ndiyo walio katika hatari zaidi na mara nyingi ndiyo wanaoathirika zaidi wakiwemo wanawake na watoto.

Kwa upande wao shirika la FAO, wao wametoa wito wamesema "kuitumia siku hii muhimu ipasavyo kutanabaisha watu kuhusu kuwa makini na kuhamasisha hatua za kusaidia kuzuia, kugundua na kudhibiti hatari zinazotokana na chakula, kuchangia uhakika wa chakula, afya ya binadamu, ustawi wa kiuchumi, kilimo, upatikanaji wa soko, utalii na maendeleo endelevu."

Hayo hayatawezekana kama hatua madhubuti zitachukuliwa baada ya maadhimisho hayo ya kila mwaka. Hatua zisipochukuliwa vizuri ni hali mbaya Zaidi itaendelea kuikumba jamii haswa iliyo katika mazingira hatarishi Zaidi. FAO wamesema.

Hata hivyo, kwa upande wa shirika la WHO limesisitiza kwa kusema "Siku hii ya kimataifa ni fursa ya kuimarisha juhudi za kuhakikisha kuwa chakula tunachokula ni salama, usalama wa chakula katika mfumo wa umma wa chakula na kupunguza mzigo wa magonjwa yanayotokana na chakula Duniani."

Kwa kutambua umuhimu wa kuhakikisha usalama wa chakula Duniani kote FAO pia imezindua nyenzo za kina za vitendo na zinazoweza kufikiwa zilizoundwa ili kuwasaidia wale wanaofanya kazi katika sekta ya chakula ili kuzangatia viwango vya kimataifa vya usafi wa chakula. Siku ya usalama wa chakula huazimishwa kila mwaka Juni 7 tangu ilipopitishwa mwaka 2018.

Sasa tumeona kuwa mashirika ya kimataifa na taasisi za kitaifa wanajitahidi sana kufikisha taarifa mbalimbali kwa kutumia maadhimisho. Swali, je yanaishia haya mambo na taarifa katika maadhimisho, au jamii inafikiwa na hatua zinachukuliwa?

Naomba tujadiliane kwa kina kwa maoni yako na ushauri ili kubadilisha jamii yetu ya Tanzania.

Vyanzo vya habari: Siku ya usalama wa chakula duniani yaadhimishwa na UM ikihimiza viwango bora huokoa maisha

Na TBS KUADHIMISHA SIKU YA CHAKULA SALAMA DUNIANI JUNI 7 , 2023 NA KAULI MBIU " VIWANGO VYA CHAKULA HUOKOA MAISHA ".
 

Attachments

Upvote 2
Back
Top Bottom