Haya huyo wenu wa CIA mnayemuami kwamba ni mkweli, aletwe sakata la Tundu Lisu!

Asante kwa maelezo mazuri,
Wenzetu linapokuja swala la investigation wapo vizuri Sana,
Nakumbuka bbc walimwelezea FBI director aliyekuja Kushughulika na shambulio la Nairobi, Alisema haikuwahi kuijua Kenya kiu jumla, na hata haikuwahi kusikia neno Nairobi,

Ila siku mbili baada ya jamaa KuingiaNairobi, tayari alikuwa amefanikisha kumkamata key suspect akiwa amelazwa hospitali Moja jijini hapo,
Na alikuwa, peke yake 'team solo'

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Kipendacho roho, chongo huita kengeza ndo wewe, uko so brainwashed kuwa Muzungu ni superior kwako na kwamba Muzungu can do no wrong huo ni ugonjwa wa akili kafanye therapy, siyo mimi niliyoichukuwa na kuisambaza hiyo Video Clip ni hao hao Wazungu unaowasifia na hata wao ukisoma comments zao wanashangaa pia sasa iweje uje na matusi na kejeli dhidi yetu Waafrika kwa kitu ambacho hata Muzungu anafanya?
 
Asante pia kwa kusoma maelezo yangu.
Tunajaribu kuelekezana kupitia mada zinazojitokeza katika JF kwa kwa lengo la kupeana taarifa sahihi ili kukuza ufahamu wetu.
Labda kwa nyongeza ya kile nilichosema awali huku nikichukua mwelekeo wa mwanzisha mada Barbarosa,ni kwamba Mike Pompeo anaposema wakati akiwa mkurugenzi wa taasisi ya Ujasusi ya America,CIA kuwa walikuwa wakiiba na pia kudanganya, taarifa hiyo haikutakiwa kumshangaza mwanzisha mada hata kidogo, kwani tunajua nyuma ya pazia hiyo ndiyo kazi ya taasisi ya ujasusi ya nchi yoyote hasa pale inapobidi.
Mfano halisi wa wizi wa CIA ulikuwa hivi;
Shirika la ndege la Saudi Arabia wakati fulani miaka ya 90 waliingia mkataba na kampuni ya Airbus kampuni la Ulaya ili watengenezewe ndege. Marekani, ambayo ni washirika wa karibu wa Saudia wakaja kusikia habari hiyo, wakashangaa kwa nini Saudia hawakuingia mkataba na kampuni ya Boeing ya America.
America walipowauliza Saudia imekuwaje, Saudia wakasema hawezi tena kuingia mkataba na Boeing kwa vile wao walishabadilishana mikataba na Airbus, kwa hiyo kama wangekataa ina maana wangeingia hasara kuvunja mkataba.
Cha kushangaza ile biashara ya Airbus kuiuzia ndege Saudia haikuendelea, na badala yake Boeing wakaonekana wameingia mkataba na Saudia na baadaye Boeing wakaanza kutengeneza ndege huku wakiwaacha Airbus wakilalamika kichinichini. Ilibidi walalamike kimyakimya kwa sababu wangelalamika rasmi kwa sauti kubwa mahakamani, wangeambiwa waoneshe mkataba wa mauziano waliongia.
Kumbe, kwa mujibu wa waandishi wa habari za kiuchunguzi, mkataba ambao Airbus walikuwa nao uliibwa katika ofisi yao kuu, tena katika eneo lenye usalama mkubwa. Na ikatajwa wizi huo ilikuwa ni kazi ya CIA,na ndiyo maana Boeing na Saudia wakawa na jeuri ya kuingia mkataba mpya.

Kichekesho ni kwamba linapokuja suala la kudanganya kwa taasisi za kijasusi,wanaweza kumdanganya hata rais aliyeko madarakani kama wataona inafaa kwa maslahi ya nchi au pengine yao.
Mathalan, rais anaweza kuambiwa na taasisi ya kijasusi ya nchi yake kwamba kuna mtu mmoja mwenye ushawishi katika jamii inaonekana anashirikiana au anatoa siri nyeti za nchi nje kitendo ambacho ni hatari kwa ustawi na usalama wa taifa. Na kwamba wao wameona kuwa kutokana na mwenendo wa mtu huyo, wameona ni bora AONDOLEWE KABISA. Namna watayomueleza watatumia ujanja wa kushawishi ili yeye rais aunge mkono hoja yao bila kupinga. Nyuma ya pazi asichokijua rais ni kwamba huyo mtu aliyetajwa kumbe hafanyi kabisa hayo mambo ambayo kwayo anatuhumiwa. Na kumbe taasisi ya ujasusi kumbe wanamwona huyo mtu atakuwa kikwazo kwa muundo au sera ambayo wao wanataka rais mpya atekeleze au aisimamie kwa maslahi ya nchi.
Haya mambo yanatokea nchi zote, ni ajabu lakini ni kweli.
Ahlan Wasaalan.
 
Damu ya hedhi Ni useless, haitengenezi watoto
Mkuu bila mzunguko wa hedhi mtu anaweza kuzaliwa kweli? Au kama mwanamke hatoi Hizo damu anauwezo wa kushika Mimba kweli..

Damu ya hedhi Ni uthibitisho tosha wa ovary ya Mwanamke kuwa active.
 
Mkuu!

Simultaneous USA bombings za Dar Es Salaam na Nairobi, unafahamu kuwa walikuja FBI?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawezi kujua hilo. Nimejaribu kuwaelewesha hilo naona imeshindikana. FBI wameshaombwa kwenda nchi mbalimbali kusaidia uchunguzi wa matukio ya kihalifu especially ugaidi. Naona yanang'ang'ania tu, "FBI ndani, CIA nje" "wote wanafanya investigation blah blah ". There is a reason FBI wapo chini ya Justice Dept.
 
Watu wazima hawajui tofauti ya investigation ya kawaida na espionage. Shule zetu siku hizi zinatengeneza madudu, Google ndio inaharibu kabisa, siku hizi wagonjwa wanaenda hospitali wakiwa tayari wanajifanya wanajua wanaugua nini na dosage pia. Utasikia mgonjwa anambishia daktari, "mbona Google inasema hivi na hivi" nasikia na madaktari nao wanawambia " haya kajitibu according to hiyo Google"
 
Bado narudia Tena jamaa ni smart vichwani mwao!, Sina lengo la kujikekejeli au kujidharau kama unavosema, Bali ni katika tu kukubali Hali halisi

Kuna mdau hapo juu ameelezea Mkataba wa Saudi Arabia ulioibiwa na Cia, ili kuinusuru boeing, kwa maslahi mapana ya USA, wizi kama huo unausemeaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sio lazima iwe ndani tu,hata ubalozi wao ulipolipuliwa walikuja hadi hapa,wao wana deal na matukio ambayo yashatokea kuchunguza,CIA ni intelijensia ya future events
Asante,sikutaka kumkumbusha Jambo Hilo,pengine hajui ama alikua bado mdogo pale Ale Qaida walipolipua US Embassy in Dar and Nairobi,waliokuja kuchunguza tukio Hilo ni FBI Wala sio CIA.
watu wa Lumumba wote wanafanana kuanzia mkubwa Hadi mdogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…