Haya Kombe la Dunia hilo linakuja tuanze sasa kugawana Timu za Kushabikia mapema

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Zifuatazo ni Timu za GENTAMYCINE kuelekea Fainali za Kombe la Dunia huko Urusi mwezi ujao ambazo nina uhakika zipo ambazo zitaenda hadi Robo na Nusu Fainali na hadi moja wapo kuibuka kuwa Bingwa hapo mwezi July:
  1. Argentina
  2. Germany
  3. Spain
  4. France
  5. Senegal
Karibu na Wewe uweke / utaje Timu zako ' pendwa ' Tano tu unazoziamini kuwa zitatoboa vyema huko Urusi.

Nawasilisha.
 
1.Egypt
2. Nigeria
3. Belgium
4. France
5.
 
Umejifunza mpira lini?
Mm sijajifunza mpira bali ni mshabiki wa mpira...

Kimsingi, nashabikia timu kulingana na jinsi moyo wangu ulivyoipenda timu... Sishabikii timu kwa kutizama majina makubwa ya wachezaji waliopo kwenye timu husika

Hizo timu mm nazielewa sana bila kujali zitabeba au hazitobeba title
 
1.Egypt
2. Nigeria
3. Belgium
4. France
5.

Hapo kwenye # 4 nakuunga mkono 100% ila kwa hizo zilizobaki nakuachia mwenyewe kwani ' Kiuchambuzi ' sioni kama zina uwezo wa kufanya vyema ila naheshimu sana ' Chaguo ' lako hilo Mkuu.
 

Sawa.
 
Umejifunza mpira lini?
Umesha nitisha! Wewe umesema TUCHAGUE TIMU ZA KUSHABIKIA. Ki uhalisia, hakuna timu itakayokosa kushabikiwa!
M' nashabikia England, ingawa hiyo timu, ni kama TAIFA STARS, ugonjwa wa moyo wa kufikia tu!
 
Umesha nitisha! Wewe umesema TUCHAGUE TIMU ZA KUSHABIKIA. Ki uhalisia, hakuna timu itakayokosa kushabikiwa!
M' nashabikia England, ingawa hiyo timu, ni kama TAIFA STARS, ugonjwa wa moyo wa kufikia tu!

Mtu yoyote anayeshabikia England hajui kabisa Mpira. Samahani kama nitakuwa nimekuudhi / nimekukwaza kwa hili Mkuu.
 
Hivi gentamycine unaweza hata kupiga japo danadana hata 5 hivi?
 
Halafu huko mbele unaweza ukawa mnafiki, sasa akicheza Argentina na German si unaweza kuwa mnafiki. Ile match ya Uefa kati ya madrid na juve ilinifanyaniwe mnafiki kweli manake juve nilikuwa naipenda na madrid nayo hivyo hivyo.
 
Wewe lazima tu utakuwa unajua na unaujua pia mpira. Kuna Mtu kanitajia Saudi Arabia yaani nimebaki tu mdomo wazi!
Mkuu, tatizo wewe unadhani labda kila mtu ni lazima ashabikie timu kubwa.

Unabaki mdomo wazi kisa nini?

Mimi naishabikia kwa mapenzi kutoka moyoni na siyo kufuatana mkumbo km nyie kila mtu Germany Germany Germany...
 
Mtu yoyote anayeshabikia England hajui kabisa Mpira. Samahani kama nitakuwa nimekuudhi / nimekukwaza kwa hili Mkuu.
Mkuu, kuishabikia timu hakuhusiani kabisa na kujua mpira. Ushabiki unaendana na mapenzi na hisia kutoka moyoni.

Uchambuzi wa soka ndiyo unaendana na ujuzi/elimu ya soka.
 
Hivi gentamycine unaweza hata kupiga japo danadana hata 5 hivi?

Form One hadi Form Four nilikuwa Mchezaji wa Kutumainiwa kabisa wa Timu ya Shule hapo nchi jirani tu ambako UKIMWI ulizinduliwa rasmi na Hayati Philemon Lutaya na nilicheza hadi katika Mashindano ya Shule makubwa huku mnayaita UMISETA na nilikuwa nikicheza sana nafasi za Beki wa Kulia au Kushoto ila nilipofika Kidato cha Tano kwenda cha Sita kutokana na aina ya Shule niliyokuwepo tulibahatika kuwa na Kocha wa Kizungu ambaye pia alikuwa ni Mwalimu wetu na alinibadilisha kutoka Kucheza nafasi ya Beki wa Kulia na Kushoto na sasa akanitengeneza hadi nikawa nacheza Kiungo cha chini ( yaani namba Sita ) na nakumbuka wakati huo nilikuwa nawaiga sana Marafiki zangu wachezaji mahiri wa Kibongo wakati huo Selemani Matola ' Veron ' na Waziri Mahadhi ' Mendieta ' uchezaji wao na nilitokea Kukubalika mno na Wanafunzi wenzangu hadi na Raia waliokuwa wakiniona nikicheza na nakumbuka hata katika hizo Shule zote nilikuwa napendwa na Mademu kwakuwa nilikuwa ' nakichafua / nakipiga ' sana dimbani Mkuu.

Niliachana na Mpira rasmi baada ya kumaliza Kidato cha Sita na kutingwa zaidi na ratiba zingine za Kitaaluma japo hata wakati nilipokuwa Chuo Kikuu nilijaribu Kucheza lakini sikuweza tena kuwa vizuri kama enzi zangu kwakuwa Mpira wangu mwingi nilipokuwa Chuoni nilikuwa nauchezea sana Gesti / Loji huku Waamuzi / Marefarii wakiwa ni Wahudumu wa hizo Nyumba za Kulala Wageni nilizokuwa nikiingia.

Kwa sasa huwa nikipata muda najaribu kucheza kidogo pale Leaders Club na akina Bakari Malima ' Jembe Ulaya ', Ally Yusuph ' Tigana ', Mtwa Kihwelo ' Dally Kimoko ' na Omary Kapilima ' Caminero ' au pande za Tanganyika Packers Kawe na akina Omary Mkuku, Kudra Omary na Benito John ila siko ' active ' kivile kwakuwa Kasi ya Vyuma Kukaza Kimasha sasa imeongezeka hivyo ' Mbichwa ' wangu muda wote unawaza nitawezaje kuielewa Kasi na hii Falsafa ya Maisha ya Rais JPM.

Ni hayo tu Mkuu.
 
1. Simba SC
2. Liverpool FC
3. FC Barcelona
4. Mabwepande Veterans

Una uhakika kabisa kwamba Bange / Bangi uliyoivuta leo ilikuwa sahihi kwa matumizi kamili ya Mwanadamu Mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…