Pre GE2025 Haya mabango ya Kisiasa yaliyosambaa Mitaani kabla ya Kampeni, je Wapinzani nao wakitaka kuweka wataruhusiwa?

Pre GE2025 Haya mabango ya Kisiasa yaliyosambaa Mitaani kabla ya Kampeni, je Wapinzani nao wakitaka kuweka wataruhusiwa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kuna suala linalonitatiza na kuleta kero kwa wananchi kama mimi, nalo ni wimbi la mabango yanayoendelea kuwekwa kila kona yakimsifu Rais, kiongozi wa chama tawala, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mafanikio ya serikali yake. Mabango haya yameenea kwa kasi, na ni ya chama tawala pekee, bila kuonesha changamoto zinazowakabili wananchi.
1729604109145.png

photo_2024-10-16_12-45-04.jpg
Najiuliza umuhimu wa mabango haya hasa tunapoelekea kwenye uchaguzi. Kwa nini mabango haya yanajitokeza kwa wingi sasa, na je, yana lengo la kutoa taarifa au kuna lengo jingine la kisiasa? Kusambaa kwa mabango haya yanayoonesha mafanikio ya chama tawala tu, kunatupa hisia kuwa hii ni kampeni za mapema, wakati ambapo sheria za uchaguzi bado hazijaruhusu kampeni.

Soma, Pia: Haya mabango ya Mama Samia kila kona, nani anagharimia? Yanatusadia nini kama nchi?

Je, hii si njia ya kujipatia faida ya kisiasa mapema kwa kutumia rasilimali za umma? Wananchi kama mimi tunahitaji kutafakari mwelekeo wa matumizi ya rasilimali zetu, hasa wakati masuala muhimu kama huduma za kijamii bado hayapatiwi ufumbuzi wa kudumu.

Kama mabango haya yana lengo la kuhamasisha maendeleo, mbona yanaelekea upande mmoja pekee wa kisiasa? Hili linanipa wasiwasi, hasa kwa wananchi wanaohitaji mazingira ya haki katika uchaguzi ujao.
 
Back
Top Bottom