Kama kuna ushahidi kwamba kweli walibaka watoto wa umri wa miaka sita na nane hilo halisahemeki, labda siku ya hukumu ya Mungu lakini sio ya hapa duniani. Yaani hao ni wa kuozea kwenye jela mpaka wafe. Japo nimesema kama kuna ushahidi, isije kuwa kulikua na kizungumkuti cha kuwaonea hao jamaa. Labda jamaa hawakufanya hicho kitu, iwe kuna mtu aliwacheza na kuwambambikizia, maana nategemea hadi rais afikie kuwapa msamaha lazima usalama wa taifa walichunguza kwa kina.
Kuna makosa ya kusamehe, hata wauaji husamehewa, lakini walawiti wa watoto wadogo, bora ufie jela.