Haya maisha sio poa kwakweli

kwanza, roho ya kulalamika, inaonekana hata ungekuwa na phd ungelalamika, tosheka na hapo,jitie nguvu ridhika na katafute kazi, acha uvivu, acha dhambi.
 
Nikununulie kamba uwahi kufa? Nani kakwambia ni dhambi?
 
Kwani umechelewa kuanza kulima?!
 
UNYAMA SANAAA
 
Miaka 24 unalialia tu.
Mimi miaka 24 ndio nilikuwa namalizia form four.
VETA umesomea nini?
Wewe ndo umewini kuliko hao wanaomaliza vyuo vya makaratasi
 
Kwani veta sio chuo?

Na lengo la kwenda veta lilikuwa nini?
 
Umempasha vilivyo, Kuna vijana wa ovyo, utakuta hata wenzake aliowaacha darasa la 7 tayari wameshaanza maisha na Wana familia zao, yeye Bado anategemea ndugu
 
Unaamini kuwa wazazi wote Wana uwezo huo wa kupiga simu sehemu ?
 
Safi , huo ndio mtazamo chanya
 


Bado u mdogo sana, jifunze hata kutengeneza boda, na Maguta, nimeona vijana wadodo wanabadili maisha na kuwa very strong financial.

Nitakupa mfano:

Haoo Nyuma nilikuwa na maguta 10, na fundi mmoja hivi ana ya service kila wakati.

Baada ya mda fulani hivi akawa hayupo makini, madereva wanalalamika.

Siku moja nikamkuta Mdogo wake ndo kwanza anajifunza tengeneza katokea Tanga.

Yule Bwana mdogo alikuwa makini mno nikampenda, nikaongea naye sana.

Nikamwambia amwambia kaka yake anataka kurudi Tanga, nikampa laki 1 nikamwambia ukifika Tanga nipe niongee na wazazi wako.

Akarudi kwao, nikaongea na wazazi wake wamruhusu aje, awe ana deal na maguta yangu,wakakubali kwa malipo fixed.

Nikafungua ka workshop hivi nikamweka hapo, basi akawa anahangaika na maguta yangu hapo.

Baada ya mda, ile frame akaanza wek vifaa vya guta, pikipiki, kwa sasa dogo kajenga self 3 bed rooms, ana vijana 4, duka kubwa, mke na watoto.
 
Tunapoelekea sijui watoto wetu watakuaje, akili.zero na hawana uvumilivu
Hali inazidi kuwa mbaya, tunawadekeza watoto sana, hawafanyi chochote Cha kuwafikirisha, miaka 24 kijana amgetakiwa tayari amejitegemea at least Kwa kula
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…