Haya makanisa ya 'manabii', 'mitume' yalianza lini hapa Tanzania?

Haya makanisa ya 'manabii', 'mitume' yalianza lini hapa Tanzania?

mshamba_hachekwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2023
Posts
20,704
Reaction score
66,337
Hii post haina lengo la kumdhihaki mkristo yeyote atakaeisoma, wala kujaribu kulinganisha imani zozote.

Ningependa kujua kutoka kwa yeyote anayefahamu mwanzo wa haya makanisa maarufu ya mitume au manabii watenda miujiza. Labda unajua, ama ulikuwepo kipindi hicho.
 
Hii post haina lengo la kumdhihaki mkristo yeyote atakaeisoma, wala kujaribu kulinganisha imani zozote......

Ningependa kujua kutoka kwa yeyote anayefahamu mwanzo wa haya makanisa maarufu ya mitume au manabii watenda miujiza..... labda unajua, ama ulikuwepo kipindi hicho........
Serikali inawalea hawa na kibaya zaidi wanawafanya waumini wajinga kinyama.
 
""mama huyu anasema nyuma hakuwa na kazi wala nyumba na elimu yake ni darasa la saba lakini baada ya kuanza kutumia mafuta sasa amepata nyumba na kazi..."""
Aiseee!!!!
 
Hawa ma aposto wengi wao hawahubiri kuacha dhambi bali ni mamotivashonspika.

Wanasaikolojia kubwa ya kuwakamua waumini hatari
 
""mama huyu anasema nyuma hakuwa na kazi wala nyumba na elimu yake ni darasa la saba lakini baada ya kuanza kutumia mafuta sasa amepata nyumba na kazi..."""

😂😂😂
Ninyi vijana WA siku kazi mnaijua Sana.
Mnavipaji vya kuchora Watu.

Eleweni Maisha kuna Wakati yanahitaji maigizo ili wengine mkono uende kinywani.
Msichukulie Serious tukisema tunaongea na Mungu
 
Pamoja na yote yanachangia kuibadilisha Jamii iwe na tabia njema. Mtu akiwa mfuasi angalau ataona aibu kufanya dhambi
Mmmmh! Hao mitume na manabii hawahubiri chochote kuhusu toba na ondoleo la dhambi wao wanasisitiza miujiza ya utajiri afya na ati siku hizi hata umeme nao unaombewa usikatike na Banka nazo hupigwa miujiza na mara huwa Matango nionavyo mitume na manabii wamesababisha uwepo wa uvivu umaskini na ujinga wa sgr miongoni mwao wanajamii si ajabu kumwona kahaba akienda kwa nabii au mtume akitaka muujiza wa kupata Madanga wa kizungu na wenye pesa bila shaka nabii atasema bwana na akupe hitaji la moyo wako
 
[emoji1][emoji1]
 
Nadhani walianza baada ya TAG na EAGT kujitenga. Ndipo akina Apostle Maboya walipoibukia.
 
Hii post haina lengo la kumdhihaki mkristo yeyote atakaeisoma, wala kujaribu kulinganisha imani zozote.

Ningependa kujua kutoka kwa yeyote anayefahamu mwanzo wa haya makanisa maarufu ya mitume au manabii watenda miujiza. Labda unajua, ama ulikuwepo kipindi hicho.
Chanzo Cha kuibuka kwa dini za kimitume. Naweza sema NI mgogoro wa TAG na EAG(T).

Hawa laiti wasingeitalafiana Hawa kina mwamposa wasingekuwepo.

List fupi.

Lusekelo NI zao la EAG(T)
Mwamposa n zao la maboya na maboya NI zao la EAG(T)

Mwisho kabisa kanisa la EAG(T)
Linaongoza kwa kutoa/kuzalisha hao manabii
 
Back
Top Bottom