Haya makosa katika uandishi wa kiswahili mbona yanashamili?

Haya makosa katika uandishi wa kiswahili mbona yanashamili?

Grahnman

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2017
Posts
1,877
Reaction score
2,550
Habari za asubuhi wana JF?

Kumekuwa na tatizo la kiuandishi kwa watu wengi kuanzia humu JF mpaka kwingineko kote kwenye mitandao ya kijamii mwanzo nilidhani ni kujisahau lakini sasa naona kama imezoeleka na kuonekana kama ni maneno ya kawaida kwenye kiswahili na watu wala hawastuki kuona kama ni makosa,yaani makosa yakirudiwa rudiwa mara nyingi huzoeleka na kuonekana ni usahihi

Naomba nitoe mifano michache ya hayo maneno hapa chini;
Nisamee badala ya Nisamehe
Eshima badala ya Heshima
Asubui badala ya Asubuhi
Mdogo angu badala ya Mdogo wangu
Kiac badala ya kiasi
Awez badala ya Hawezi
Ujaacha badala ya Hujaacha
Uendelei badala ya Huendelei
Utamsikia Mtangazaji anasema Nyimbo hii badala ya kusema wimbo huu

Yako maneno mengi sana yanayopotoshwa na wadau wengi humu ndani,ombi langu tu ndugu zangu tubadilike tuandike maneno kwa usahihi wake kwa sababu humu ndani panapitiwa na wanafunzi kuanzia Shule za Msingi,Sekondari na hata Vyuo wanajifunza nini juu ya tunayoyaandika humu?

Eti hapo ndio tunawadharau Wakenya hawajui Kiswahili hawajui kiswahili wakati sisi wenyewe ndio tunavuruga tu.

Ni hayo tu wadau muwe na Jumapili njema.
 
Pooh! ivi mboni uko ivo wewe unaakiri kweli? Tusipojua kuandika kiswairi asara kwa nani?harafu sio vizuli eboo!! (in Bi Chau's Voice mtangazaji mwandamizi kipindi cha JUNGU KUU ITV)
 
Pooh! ivi mboni uko ivo wewe unaakiri kweli? Tusipojua kuandika kiswairi asara kwa nani?harafu sio vizuli eboo!! (in Bi Chau's Voice mtangazaji mwandamizi kipindi cha JUNGU KUU ITV)
Ha ha ha ha!!
 
Back
Top Bottom