Haya mliowahi angalia hizi movie tujuane

Aiseeeh hiyo ndo ilikuwa raha zetu, enzi hizo home hakunw TV CHOGO
 
Unachota maji pipa moja unalipwa shingi 150 kiingilio tayari...
 
Hahahaa sure, wale wajeshi waliokuwa wanakuja kwa wingi halafu komandoo anawamiminia risasi huku akipiga kelele hiyaaaaa hiyaaaaa kamoni kamoni ngi ngi ngi ngi ngi ! Sie tulikuwa tukiwaita WAROMBO
Filamu hizi za watasha na wachinese(Hong Kong) aisee nilipata kuzitazama sana,

Mfano movi likiisha mnatoka nje mkiwa na shangwe tele mukichora hewani mastyle ya karatee wakati mwingine rafiki zako wakizingua unawachorea za mai faza izi hiro au sneki mankeyi shado.

Inkridibo kungufu misheni bonge la muvi enzi za akina Alexander Lou na Jonh -Lee(mguu mmoja hewani kama dakika tano).

Filamu za kihindi za Mituni na mbabe wa india Sanny Deo,Amita ,Amri Khan,zlilinibamba sana.Sasa miaka ya nyuma kidogo sinikataka tunda la toto la kihindi kwa mtaa wa- wahindi ghafla kaka zake wakaniijia juu kama moto wa kifuu na mikwaraa kibao,nikawaambia nyinyi mbona mnatafuna dadazetu mambo yanakuwa poa tu,kwetu sisi mbona inakuwa nongwa...??
Kidume nikasema hamnitishi na mikawara yenu ya mbuzi hapa jino kwa jino, jicho kwa jicho kama vita ya ukomonosti na ubepari.

Naashukuru filamu hizi za utotoni zimenisaidia kwa kiasi flani kuwa na vinasaba vya udadisi wa mambo mbali mbali ulimwenguni.

No ritriti no sarrenda 2,Kubwa la maadui lilikuwa na nguvu za ajabu jamaa lina vuta gari na bwawa kubwa la Mamba(mifugo).

Phantom-Vietnam,

Napigana na maadui mbona hawaaishi ooohh kumbe wavietnam.
 
Mkuu umenikumbusha mbali hiyo phantom soldiers ilikuwa balaa,jamaa yanaua kisha yanapunga mikono hewani [emoji2]
 
Mkuu umenikumbusha mbali hiyo phantom soldiers ilikuwa balaa,jamaa yanaua kisha yanapunga mikono hewani [emoji2]
Hatari sana.

Wanavamia kijiji na kuteketeza chote kisha wanaweka Fuvu la binadamu kama alama yao kwamba vidume vya mbegu vimepita mahali hapa.

Risasi hazipenyi mavazi yao.
 
Hatari sana.

Wanavamia kijiji na kuteketeza chote kisha wanaweka Fuvu la binadamu kama alama yao kwamba vidume vya mbegu vimepita mahali hapa.

Risasi hazipenyi mavazi yao.
Ila Hollywood zamani walikuwa wanatoa action kali sana siku hizi hizo sci-fi zimezidi kiasi ladha imeondoka kama sio kubaki kidogo,uhalisia haupo kiviile.
 


Enzi za hizi makitu nilitumia fursa sana.... nlikua nazama na deli langu la aisikirimu... nikitoka nna buku2 za enzi hizo..... mambo yakaanza kunichachia nlivoanza twisheni wakat nimeingia la saba.... dah...

Sitasahau siku nimeingia jamaa wakanipa sijui ilikua hela ya wapi ile walah(si unajua mule ndani giza)...... wakchkua ashkilimu kumi........

Any ways, saiv huwa nainjoy kuchek muvi peke yangu, hasa nyakat za usiku.
 
Hapo kama bi mkubwa ndo alikutuma lazima ulikula stiki uliporudi home.
 
Movie za Jet Li
Taichi
Taichi Master
Romeo Must Die
The Boardguard from Being
The Black Mask
Fearless
The Forbidden Kingdom
The Invisible Shaolin
The Mummys Tomb of Dragon Emperor
The One
Kiss of the Dragon
Once Upon a time in China
Fist of Legend
Shaolin Temple
 
Ila Hollywood zamani walikuwa wanatoa action kali sana siku hizi hizo sci-fi zimezidi kiasi ladha imeondoka kama sio kubaki kidogo,uhalisia haupo kiviile.
Ndio ndio Mkuu,

Hivi sasa nimekuwa mvivu sana kutazama movi za Hollywood na Bollywood na Nollywood, hata Bongowood za nyuma hasa za kichawi na madubwana (zogo,kinyamkela) nilizitazama sana. Zote nimekuwa mivivu sana.

Sci-fi movies unakuta zimejaa Aliens na vitu vya ajabu (Matrix).

Unakuta mtu anapigwa ngumi ubungo anaenda kuangukia kibaha.
 
Wazee wa Pilau mpoooo mida flaan hv ya night Kali
 
Aaah nimekumbuka mbali sana enzi za vibanda ushenzi, nlikua nakula bakora kila siku kisa komando kipensi dah
 
Aaah nimekumbuka mbali sana enzi za vibanda ushenzi, nlikua nakula bakora kila siku kisa komando kipensi dah
Tofauti ya zamani na siku hizi zamani unaeza tazama muvi moja hata mara 3 kwa wiki,zama zimebadilika
 
I have watched all...ila hivyo ya yaya sio Amita ni Govinda yaya adui Ranjit
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…